Saturday, January 17, 2015

HABARI KUBWA LEO,NECTA WATANGAZA MATOKEO

Pichani niKatibu Mkuu wa Baraza la Mitiani nchini NECTA Dkt Charles E Msonde Akizungumza leo na Waandishi wa Habari jijini Dar Es Salaam 

NA KAROLI VINSENT
BARAZA la Mitihani nchini NECTA limetangaza matokea ya kidato cha pili yaliyofanyika mwaka jana 2014 huku idadi kubwa ya wanafunzi wakiwa  wamefaulu na kujiunga kidato cha tatu, ikiongeza kwa asilimia 92.66 ikilinganisha na mwaka 2013 ambapo idadi ya wanafunzi waliofaulu ilikuwa asilimia 89.34.
       Matokeo hayo yametangazwa leo Jijini Dar es Salaam na Katibu Mkuu wa Baraza la Mitihani nchini NECTA Dkt Charles E Msonde wakati wa mkutano na waandishi wa Habari ambapo alisema watahiniwa  waliofanya mtihani huo uliofanyika mwezi Novemba mwaka jana ilikuwa 405,204 sawa na asilimia 89.40 Kati ya hao wasichana walikuwa 233,834 sawa na asilimia 51.60 na wavulana walikuwa  219,357 sawa na aslimia 48.40.
     
Dkt Msonde alisema kati ya watahiniwa hao waliofaulu na kupata alama na kuweza kuendelea na kidato cha tatu walikuwa 375,434 Sawa na asilimia 92.6 ya watahiwa wote waliofanya mtihani huo ambapo wasichana walikuwa 195,328 sawa na asilimia 92.8 na wavulana 180106 sawa na aslimia 92.69.
       
 Aidha,Dokt Msonde aliwataja watahiniwa ambao wamepata alama ambazo hawawezi kuendelea na kidato cha Tatu na  itawanalazimu kurudia kidato cha pili walikuwa 29770 kati ya asilimia 7.34.
      Vilevile ,Dokta Msonde aliyetaja masomo waliofanya vizuri wanatahiniwa hao ni ya Uraia,Historiya,Kiswahili,kingeleza,jeografia


Waandishi wa Habari wakimsikiliza kwa Makini 

 Pia Masomo waliofanya vibaya watahiniwa hao ni ya  Hesabu,Kemia,kilimo,Somo la Biashara pamoja na Biolojia.
Alibanisha kuwa sababu iliofanya idadi ya wanafunzi mwaka huu kuwa mazuri  imetokana na mipango mizuri ya serikali huku ikizingatia sasa kuwepo na mfumo mpya wa matokea mkubwa sasa na akawata walimu na wazazi waendele kutoa mshikamano kwa walimu.

Matokeo yote ya Kidato cha pili yatakuwepo kwenye Mtandao wa baraza la Mitiani nchini,tovuti ya Wizara ya Elimu na Ofisi ya Wzari Mkuu Tamisemi, pamoja na Kwenye shule husika ya Mwanafunzi anayesoma. 
MTANDAO HUU PIA UTAKUPA MATOKEO HAYO PINDI TU YATAKAPOTUFIKIA

No comments: