Friday, January 23, 2015

HATARII--DAWA HATARI ZAINGIA SOKONI,TFDA YATANGAZA KUZIFUNGIA MARA MOJA,SOMA UZIJUE DAWA HIZO

Pichani ni Mkurugenzi wa Mamlaka ya Chakula na Dawa nchini TFDA Bwana
 Mitangu Adam Fimbo akizungumza na waandishi wa habari leo
Jijini Dar Es Salaam 
NA KAROLI VINSENT

         MAMLAKA ya Chakula na Dawa nchini (TFDA) imezifutia Usajili na kuzuia Uingizaji Dawa tano  za Binadamu kutokana na kuwepo makosa mbalimbali.
      
              Hayo yametangazwa leo jijini Dar es Salaam na Mkurugenzi mkuu  wa Mamlaka ya Chakula na Dawa nchini (TFDA) Mitangu Adam Fimbo Wakati wa Mkutano na Waandishi wa Habari ambapo alisema Mamlaka hiyo katika kupitia mifumo ya ufuatiliaji  wa usalama na ubora wa dawa nchini wamebaini uwepo wa dawa duni kwenye soko zenye madhara na zisizofaa kwa matumizi ya Binadamu.
        
            Ambapo katika kufuatilia huko,Mamlaka hiyo  imefikia hatua ya kufuta   usajili wa aina tano za dawa za binadamu ,ambazo ni Dawa ya kutibu “Fungus” ya vidonge na kapsuli aina ya ketocanazole ambayo mamlaka hiyo imesema sababu ya kuzuia kwake ni kutokana na kubaini dawa hiyo inasababisha madhara hatarishi katika Ini kwa watumiaji.
         
          Na nyingene ni dawa ya kutibu malaria ya maji na vidonge aina ya Amodiaquine nayo pia  Mamlaka hiyo imesema sababu ya kufutia usajili na kuzuia kuingia nchini kutokana na mabadiliko ya mwongozo wa kisera wa kupima na kutibu malaria wa mwaka 2013 wizara ya Afya na Ustawi wa jamii ambapo mabadiliko hayo yamebaini Amodiaquine ikitumika peke yake inaleta usugu wa vimelea vya malaria.
       
            Mkurugenzi huyo aliitaja dawa nyingine Dawa ambayo ni hatari kwa binadamu ni Dawa ya  kutibu mafua na kikohozi za Maji,Vidonge na kapsuli zenye kiambato hai aina ya Phenylpropanol amine ambacho anasema kinaleta madhara hatarishi kwa binadamu kama vile kiharusi (Hemorrhagic sroke).
          
        Mbali na hizo Dawa zengine ni Dawa ya kuua bacteria ya Sindano aina ya Chloramphenic ol Sodiam Succinate inayotengenezwa nchini India pamoja na dawa ya kuua Bakteria ya Maji na kapsuli aina ya Cloxacillin ambazo zote kwa pamoja bwana Fimbo alizitaja kwamba zina madhara kwa watumiaji ikiwemo kushindwa kupumua na kupoteza Fahamu.
       
    Katika Hatua Nyingine mamlaka hiyo imebadili na kudhibiti aina nne ya dawa mbalimbali.
        
         Dawa hizo ni Dawa ya kutibu imebadilika matumizi yake,malaria ya vidonge yenye mchanganyiko wa Sulphadoxine na pyrimethamine na dawa aina ya Kanamycin Amikacin na Levofloxian.

      
       

Aidha Bwana Fimbo aliwataka wamiliki wa maduka ya Dawa,pamoja wananchi kuzingatia taarifa zinazotoka kwenye Mamlaka hiyo ili wasikumbane na matatizo na akazitaka Hospitali mbalimbali nchini pamoja maduka ya dawa kuaacha kuuza dawa hizo mala moja.

No comments: