.

TIZAMA REPORT NZIMA YA SAKATA LA LIPUMBA LEO,CUF WAJA JUU,MJADALA BUNGENI WAJADILIWA.


NA KAROLI VINSENT

SIKU moja kupita  baada Mwenyekiti wa Chama cha Wananchi CUF,Profesa Ibrahimu Lipumba kupandishwa mahakamani kwa kile kinachodaiwa kushawishi wanachama wa chama  hicho kuandamana na kupelekea jeshi hilo kutumia nguvu katika maeneo ya Mtongani wilaya ya temeke Jijiji Dar es Salaam.
          
Nacho Chama cha Wananchi CUF,kimeibuka na kulivaa jeshi la polisi nchini na kusema jeshi hilo linatumiwa na chama cha mapinduzi CCM,ili kudhoofisha upinzani nchi.
     
     Kauli hiyo imetolewa Leo Jijini Dar es Salaam na Kaimu mwenyekiti wa Chama cha wananchi Cuf ,Juma Duni Haji,Wakati wa Mkutano na  waandishi wa Habari ili kuzungumzia kitendo alichofanyiwa mwenyekiti wa chama hicho cha kupigwa na polisi,ambapo Bwana haji alisema Chama hicho kinalaani vikali kile alichodai ni hujuma wanachofanyiwa na polisi Kuzoofisha upinzani nchini.
        
 “Cuf-tunalaani kitendo hicho cha jeshi la polisi nchini kutumika kisiasa kuzuia shuguli halali za vyama vya upinzani nchini na kuwaruhusu ccm kufanya wanavyotaka bila kubughudhiwa na vyombo vya dola wala kisingizia vya sababu za kintelijinsia”
        
 “Kumkamata mwenyekiti wetu wa taifa,kumdhalilisha pasipo kuwepo kwa maandamano ambayo CUF na viongozi wake walishakubaliana kutofanya”alisema Bwana Haji. 
        
 Bwana Haji aliongeza kuwa licha ya kulaani kupigwa kwa mwenyekiti wao pia wanalaani kupigwa hata kupigwa wananchama wao ambao wanadai walikuwa hawana kosa lolote.
        
 Aida,Bwana Haji alibainisha kuwa hata hoja wanayoisema jeshi la Polisi kwamba chama hicho kilidharau magizo ya jeshi la Polisi,kuendelea na maandamano hayo kwa kusema sio kweli kwani chama hicho kilifuata maagizo yote.

        
Vilevile,Bwana Haji alilitaka jeshi la polisi kuacha kutumika na chama cha  mapinduzi CCM kwani wanachokifanya hakikubaliki na chama hicho kitachoka na kuongeza kuwa kuchoka huko kutapelekea Taifa kutotawalika na amani ya nchi itakuwa imevurugika
      
 Bungeni Mjadala uliendelea Hivi.


Baada ya Jana Spika Anna Makinda kuliharisha Bunge mara mbili jana ili kupisha Serikali kupeleka Taarifa kamili ya Jeshi la Polisi kutumia nguvu ya kubwa ya Mabomu kuwapiga wananchama wa CUF,waliokuwa wakiandamana kuadhimisha kumbukumbu ya Mauaji yanayodaiwa kufanya jshi la Polisi huko Zanzibar Januari 26 na 27 Mwaka 2001 na kupelekea vifo vya watu zaidi ya 30.Bunge hilo lilendelea Leo-
        
  Kwa Waziri wa Mambo ya Ndani ya nchi Bwana Mathiasi Chikawe akitoa Taarifa kwaniaba ya Serikali ambapo alisema Jeshi la Polisi lilikuwa Sahihi kutumia nguvu kuwatawanya wananchama chama cha Wananchi CUF kwa madai Jeshi hilo lilitoa taarifa za kubaini kumekuwa kunawatu wanataka kuvuruga amani kwenye maandamno hayo na chama hicho kikakaida taarifa hizo.
    
Baada kutoa Tamko hilo kwa niaba ya Serikali na pia Waziri mwenye Dhamana Jeshi la Polisi nchini.
       
 Ndipo Mwanasheria Mpya wa Serikali Gorge Masanju akamtaka Spika Anne Makinda kuacha kulizungumzia Suala hilo kwa madai tayari lipo katika Mahakama na kuendelea kufanya hivyo kugonganisha Mihimili miwili kati ya Bunge na Mahakama.
         Kauli hiyo ya AG Masanju ikapingwa na Spika makinda na Kutaka Majadala uendelee.
        
  Wabunge wakaachangia

Wabunge walipota kuchangia wa kwanza alikuwa Mbunge wa Singida Mashariki Tundu Lissu ambapo yeye alikituhumu chama cha mapinduzi CCM,kwa kulifanya jeshi la polisi kuwa watu wao na kumuomba Waziri wa Mambo ya Ndani Chikawe ajiuzulu.

“Jeshi letu letu la polisi limetekwa nyala na element la kifashisti,tena zinaungwa ndani ya CCM na serikali yake,kumbe tunapigwa kutokana na hao ambao wanasema tupigwe tu,leo nashangaa waziri chikawe na waziri mkuu kwanini wasijiulu”

“Sheria za vyama vya siasa zinasema wazi nashangaa huyo waziri chikawe anayesema ambayo atakiwi kuwepo hapo,sheria haziwapi mamlaka kuvuzuia maandamano’alisema Lissu.
      Gwiji huyo wa Masuala ya Sheria nchini ambaye pia ni Mwanasheria mkuu wa Chadema aliendelea kuongea kwa uchungu akisema hakuna mbunge wa upinzania  asiyepigwa na jeshi la polisi.
       
      “Watu wetu wameuliwa na jeshi la polisi na mwangosi kauawa na jeshi la polisi leo RPC Kamuanda aliyemua kupandishwa cheo,watu wetu wameuwa na jeshi la polisi,leo nashangaa waziri huyu anakuja kudanganya bunge hivi”

“Katika hali hii lazima bunge lifikie maamuzi la kuwajibishe hao wenye mamlaka wanao hamulu sisi kupigwa ,ambaye ni waziri mkuu,na mwengine ni Waziri Chikawe nae pia aondoke kama tulivowaajibisha majizi ya Escrow”alisema lissu.
        Kwa upande Mwenyekiti wa kambi ya Upinzani Bungeni Freeman Mbowe alisema Vitendo walivyofanya Jeshi la Polisi havikubariki na vinafaa kupigwa Vita.
    
Wabunge wa CCM wanena.

Kwa upande wao wabunge wa Chama cha Mapinduzi CCM,walitetea jeshi la Polisi na kusema kama mtu atakayekiuka sheria apigwe tu.
      
  Kwa upande wake  Mbunge wa Jimbo la Mtera Mh. Livingstone Lusinde alisema jeshi la Polisi liko sahihi kwa kitendo walichokifanya kwani viongozi wa CUF,walilenga kuvuruga Amani ya nchi.
         Hali ya  hewa yachafuka Bungeni
     
     Naye MBUNGE wa Donge, Sadifa Juma Khamis (CCM) alichafua hali ya hewa Bungeni hapo baada ya kusema Mwenyekiti wa Chama cha  Wananchi CUF,Profesa Ibrahimu Lipumba ambaye amesema amepigwa na kusema hajapigwa bali amegushwa.

“Huyo anayesema amepigwa lipumba,hivi kapigwa Yule kagushwa,eti anasema waziri ajiuzulu mtu kagushwa angepigwa angetembea Yule,eti anajifananisha rais kikwete na Lipumba na Rais wanafanana sio kweli kwani CUF ni chama ni Saccos ili ile ni Saccos’alisema Mbunge Khamis Sadifa.
  
 Spika Makinda aokoa Jahazi na kumtaka Mbunge Sadifa afute kuli yake maana fujo zilianza kutoakea bungeni Ndipo mbunge akatoa maneno ya Saccos.
        
   Mjadala ulipokwisha.

Kwa upande wake Mtoa hoja Mbunge wa Kuteuliwa James Mbatia alikubaliana na Bunge kuacha mahakama iachiwe na kusema serikali inatakiwa iondoe ukiritimba ulioko ndani ya jeshi la polisi kwa kuondoa mfumo uliopo ambao unaleta mtafaruku kati ya polisi na vyama vya siasa.
  
 Makinda anena.

Spika makinda alimaliza mjadala huo kwa kusema kanuni ya 47,inahaja kuangaliwa kwamba jambo hilo sio la dharula bali ni la muhimu na kusema mjadala huo uishia hapo na kuiacha mahakama kufanya kazi yake.

About HABARI24 TV

Post a Comment
Powered by Blogger.