Friday, January 16, 2015

WEZI WAZIDI KULITESA SHIRIKA LA TANESCO,WAIBA WAYA WENYE THAMANI YA MAMILIONI-SOMA HAPA KUJUA

Kituo kinachomilikiwa na shirika la Umeme nchini Tanesco picha na maktaba picha kamili itakujia 
NA KAROLI VINSENT
WATU wasiojulikana wamekivamia kituo cha upozaji na usambazaji wa umeme nchini TANESCO kilichopo Uwanja wa ndege Jijini Dar es Salaam na kuiba waya wenye Thamani ya Milioni 150 za kitanzania na kutokomea kusiko julikana
            Na kulifanya Shirika la Umeme nchini kukwama kuwasha Jenereta za kituo hicho ambacho walitarajia kuwanya mwezi marchi mwaka huu.
      
     Akithibitisha kutokea kwa wizi huo leo Jijini Dar es Salaam    Meneja wa ugawaji na usambazaji wa  Umeme wa shirika hilo  bwana Emmanueli Maniraboma Wakati alipotembelewa na vyombo mbalimbali vya Habari,ambapo alisema wizi huo wa waya umekwamisha mipango ya kuwasha mitambo mbalimbali ya umeme kituoni hapo.
 
“Kutokana na wizi huu tumekwama  kufanya mambo mengi yenye maendeleo katika kituo hiki,kwani tulitarajia kuwasha mitambo hii ili watumiaji wa umeme watumia  vizuri na kutokana wizi huu,sasa tumekwama kabisa”alisema Bwana Maniraboma.
   
  Bwana Maniraboma aliongeza kuwa waya hizo zilizoibia hazipatikani nchini   na mpaka kuzileta nchini ilitumia zaidi ya milioni 150 za kitanzania kwa kutumia usafiri wa meli na wakitumia usafiri wa ndege gharama zitaongezeka na kufikia fedha za kitanzania zaidi ya milioni 200.ambapo uagizaji wake utachukua zaidi ya miezi mitatu.
           
 Aidha,bwana Maniraboma alisema kutokana na wizi huo shirika limechukua hatua ikiwemo kufanyia uchunguzi juu ya hujuma wizi huo na ikibainika hatua kali za kisheria zichukuliwe kwa walinzi wanaorinda kituo hicho.

         Kwa upande wake Afisa Mwandamizi wa sheria na Uchunguzi wa Shirika la Umeme TANESCO lenin Kiabya alisema kwa sasa wako kwenye uchunguzi ikiwemo kwa walinzi wanaorinda kituoni hapo na ikibainika kama wao walizembea mpaka wizi huo kutokea watachukuliwa hatua kali za kisheria

No comments: