Friday, March 6, 2015

SENTENS TANO WALIZOTOA TMA LEO KUHUSU MAAFA YA MVUA HUKO SHINYANGA

Baada ya maafa yalitokea huko mkoani shinyanga yakihusisha mvua kubwa iliyokuwa inanyesha mapema wiki hii mamlaka ya hali ya hewa kupoitia mkurugenzi wake  bi AGNES KIJAZI amezungumza na mwandishi wa mtandao huu na kutoa machache kuhusu kile ambacho kilitokea na hatua ambazo walikuwa wakizichukua

1-Kwanza ndugu mwandishi kilichotokea mkoani shinyanga ni kitu ambacho kinaitwa TONADO ambayo ni kitu ambacho sio mara nyingi kutokea katika ukanda wa nchi zetu za africa.
2-TONADO ni mkusanyiko mkubwa wa mawingu uliozidi kipimo ambao huwa angani ambao ukizidi ukianza kuanguka ndio unaitwa jina hilo,narudia kuwa sio mara nyingi kitu kama hichi kinatokea duniani.

3-Hii imetokea kwa sasa nadhani ni kutokana na mabadiliko ya hali ya hewa ambayo yanaanza kutokea mambo ambayo yalikuwa hayatarajiwi kutokea japo yapo duniani.

4-Tuliona wingu nzito katika ukanda ule na katika utabiri wetu wa saa 24 wa siku ile tulitangaza japo lilikuwa ni wingu la kawaida sana hatukujua kama linaweza kuzaa TONADO,lakini ilipokuwa inaenda usiku zaidi tulianza kushtuka baada ya kuona wingu linazidi na tukawa hatuna njia yoyote ya kuchukua tahadhari tena na ndio kikatokea kilichotokea.

5-Wananchi wa maeneo mengine wasiwe na wasiwasi kwani TONADO haitokei mara kwa mara na hadi sasa hatuna taarifa za maeneo mengine ambayo linaweza kutokea tatizo kama hilo

No comments: