Friday, March 20, 2015

FAHAMU ALICHOKIFANYA KAMISHNA KOVA LEO JIJINI DAR ES SALAAM


Jeshi la Polisi Kanda Maalum ya Dar es Salaam linawashikilia watu wawili wanaojiita ni viongozi wa watu waliopitia mafunzo ya mgambo kwa kosa la kuratibu na kuongoza vikao vya uchochezi vya mgambo dhidi ya serikali.

Watuhumiwa hawa wanajulikama kwa majina ya MATHIAS S/O LUBEGA, Miaka 43, Mkazi wa Bunju, aliyekamatiwa Mission Pub maeneo ya Mbagala Mkoa wa kipolisi Temeke. Wa pili anaitwa MG 437236 MOHAMED S/O ALLY, Miaka 28, Mkazi wa Mbagala Zakhiem ambaye alikamatiwa maeneo ya Temeke alikokuwa amejificha. 

Watu hawa wamekuwa wakikutana mara kwa mara jijini Dar es Salaam kwa lengo la kupata idadi kubwa ya wanamgambo ambao watawaunga mkono katika malengo yao. Pia wamekamatwa na nyaraka mbalimbali za uchochezi zenye lengo la kuwashawishi wanamgambo kuamka na kutambua kuwa wananyimwa haki zao na serikali.

Taarifa za awali zinaonyesha kwamba lengo lao kuu ni kuwakusanya kuwapotosha wenzao ili kuleta uvunjivu wa amani kupitia madai ambayo hayana msingi wowote wa kisheria.

Natoa wito kwa wanamgambo wote waendelee kuwa waadilifu na kuzingatia mafunzo yao ya uzalendo na ukakamavu na kuwa tayari kuitumikia nchi yao kutokana na maelekezo na sio kwenda kinyume na hapo.

MAJAMBAZI SUGU SABA WAKAMATWA NA SILAHA JIJINI DAR ES SALAAM


Katika hatua nyingine Jeshi la Polisi Kanda Maalum linaendesha oparesheni kamambe katika maeneo yote ya jiji la Dar es Salaam ambapo limepata mafanikio kam ifuatavyo:

1.    KUKAMATWA KWA SILAHA NA WATUHUMIWA WA UJAMBAZI

Kuanzia tarehe 05/03/2015 hadi sasa zimekamatwa silaha tatu aina tofauti na watuhumiwa saba wakihusishwa na silaha hizo wakizitumia katika matukio mbalimbali ya ujambazi.
Tarehe 06/03/2015 huko Mwananyamala ilikamatwa Bastola aina ya REVOLVER yenye namab 106108074 TZCAR96093 ikiwa na risasi 12 pamoja na watuhumiwa watatu. watuhumiwa hawa walikamatwa baada ya kupatikana kwa taarifa toka kwa msiri. Watuhumiwa hao ni:

a:  RAMADHANI S/O MASANJA MHAMBO, Miaka 34, Baharia, Mkazi wa Mwananyamala.
b: ELIAZR S/O JACKOB NKURARUMI @ JUMA ADAM MOHAMED, MRUNDI, Miaka 25,  Mlinzi wa Colombia Hotel, Mkazi wa Tandale.
c: RAJAB S/O NASSORO, Miaka 30, Fundi Simu, Mkazi wa Mwananyamala kwa Sindano.
Aidha tarehe 07/03/2015 maeneo ya Mbagala kizuiani walikamatwa watuhumiwa wawili wakiwa na bunduki moja aina ya SHORTGUN PUMP ACTION yenye namba R216145 TZCAR79067 ikiwa na risasi mbili. Watuhumiwa hao ni kama ifuatavyo:
a: SAID S/O ZUBER  KIBWANA @ BAKHRESA, Miaka 33, Mkazi wa Mbagala.
b: OMAR S/O NZEGULA MPONDAMALI, MIAKA 29, Mkazi wa Kigamboni Mikwambe.

Watuhumiwa wengine wawili walikamatwa wakienda kufanya tukio maeneo ya Namanga Mkoa wa Kipolisi Kinondoni lakini waliwekewa mtego na polisi na kukamatwa kabla hawajafanya tukio hilo. Walikamatwa wakiwa na Bastola aina ya BROWNING COURT yenye nambari A558651 na risasi kumi. Watuhuniwa wananendelea kuhojiwa ili sheria ichukue mkondo wake.

KUKAMATWA KWA DOLLA ZA KIMAREKANI ZIPATAZO 426 ZINAZODHANIWA KUWA NI BANDIA.

Aidha, msako huu unaoendelea umefanikisha kukamatwa kwa noti bandia za Dolla za Kimarekani zipatazo 426 ambapo noti 36 ni za Dolla 100 na noti 390 ni za Dolla 50.
Dola hizi bandia zimekamatwa kwa watuhumiwa RAMADHANI S/O MASANJA MHAMBO, Miaka 34, Baharia, Mkazi wa Mwananyamala; ELIAZR S/O JACKOB NKURARUMI @ JUMA ADAM MOHAMED, MRUNDI, Miaka 25,  Mlinzi wa Colombia Hotel, Mkazi wa Tandale; na
RAJAB S/O NASSORO, Miaka 30, Fundi Simu, Mkazi wa Mwananyamala kwa Sindano, walipopekuliwa kwenye makazi yao.
Noti hizo zikibadilishwa katika pesa za kitanzania ni sawa na shilingi za kitanzania 42,504,000/= (Millioni arobaini na mbili, mia tano na nne elfu)

Jeshi la Polisi linawatahadharisha watanzania kuwa makini wanapofanya manunuzi au biashara yoyote kwa sababu wanaweza kuangukia katika mtego wa kupewa noti bandia.

No comments: