Wednesday, March 25, 2015

JUKATA WABAINI RUSHWA KATIKA UANDIKISHWAJI WA DAFATARI LA WAPIGA KURA NJOMBE

RUSHWA.
Viongozi wa JUKATA wakiongozwa na kaimu mwenyekiti HEBRON MWAKAGENDA wakizungumza na wanahabari mapema leo
Wakati serikali kupitia tume ya taifa ya uchaguzi ikiendelea kurattibu mchakati wa uandikishwaji wa daftari la kidumu la wapiga kura kwa mfumo wa BVR zoezi ambalo lilianzia katika miji ya  njombe,tuhuma za rushwa zimeibuka katika mchakato huo.

Akiibua tuhuma hiyo kaimu mwenyekiti wa jukwaa la katiba tanzania JUKATA bwana HEBRON MWAKAGENDA amesema kuwa kumekuwa na vitendo kadhaa vya rushwa katika zoezi hilo ambapo baadhi ya wananchi wamekuwa wakitoa rushwa ili kuandikishwa mapema katika zoezi hilo baada ya kusota kwenye foleni kwa muda mrefu .

Amesema kuwa ktokana na upungufu wa vifaa katika zoezi hilo ambapo watu zaidi ya 26000walitakiwa kujiandikisha ambapo mashine za kufanya kazi hiyo zilikuwa 38 tu jambo ambalo lilipelekea usumbufu wa wananchi na wengine kuamua kususia zoezi hilo.


Ameongeza kuwa utafiti ambao ulifanywa na jukwaa hilo kuanzia tarehe 18 hadi 22 mwezi wa tatu unaonyesha kuwa hali bado ni tete na ni kata moja tu ya YAKOBI iliyoonekana kukamilisha zoezi hilo kwa asilimia 80 wakati kata nyingine zikiendelea kusua sua,ambapo amesema hadi sasa wananchi waliofanikiwa kujiandisha mpaka tarehe 22 mwezi wa tatu kwa kata zote walikuwa 17000 na hivyo wananchi zaidi ya 9000 wamebaki bila kujiandikisha.


Ameongeza kuwa kumekuwa na habari ambazo ni za kiuaminika kuwa serikali inajiandaa kuendesha zoezi la kura ya maoni kwa kutumia daftari la kudumu la zamani ambalo kwa mujibu wa mwenyekiti wa tume ya taifa ya uchaguzi jaji DAMIANO LUBUVA anasema kuwa daftari hilo limechafuka sana na halifai kiasi ambacho haliwezi kurekebishika tena.

No comments: