Wednesday, March 25, 2015

JUKWAA LA KATIBA WAIBUKA UPYAAA--SASA WATAKA MCHAKATO WA KURA YA MAONI USIFANYIKE,SOMA WALICHOKISEMA LEO


Kaimu mwenyekiti wa jukwaa la katiba Tanzania ndugu HEBRON MWAKAGENDA akizngumza na wanahabari muda mfupi uliopita juu ya mchakato wa upatikanaji wa katiba mpya ambapo amesema kuwa hakuna matumaini wala mawazo ya kupata kwa katiba mpya Tanzania kwani kuna mapungufu mengi sana katika mchakato huo na serikali imefikia mwisho wa mawazo yake na imebaki kuwadanganya watanzania juu ya mchakato huo
 Jukwaa la katiba tanzania JUKATA wameitaka serikali kuahirisha mchakato mzima wa upatikanaji wa katiba mpya hadi mara baada ya uchaguzi mkuu wa Tanzania mwaka huu kwa kile walichodai kuwa ni mchakato huo kujawa na mapungufu mengi ikiwemo maandalizi  mabovu yanayofanyika kuelekea katika upigaji wa kura ya maoni juu ya katiba pendekezwa.
Akizungumza na wanahabari mapema leo jijini Dar es salaam kaimu mwenyekiti wa jukwaa hilo ndugu HEBRON MWAKAGENDA amesema kuwa kusuasa sua kwa zoezi la uandikishwaji wa daftari la kudumu kwa mfumo mpya wa BVR,ni ishara tosha kuwa ni ndoto kwa Tanzania kupata katiba bora kwani hadi sasa kuna idadi kubwa ya wananchi ambao hawajajiandikisha katika daftari hilo huku muda wa kupiga kura hiyo ukiwa unakaribia jambo ambalo limekuwa likimtatiza kila mtanzania kama jambo hilo linawezekana.
Amesema kuwa kutokana na upungufu wa vifaa pamoja na rasilimali nyingine unaoonekana wazi katika zoezi hilo ni wazi kuwa daftari hilo haliwezi kukamilika na kutumika katika kura ya maoni ya katiba.

Amesema kuwa zoezi ambalo lilifanyika katika miji ya makambako na njombe la uandikishwaji wa daftari hilo limeonekana kuchukua zaidi ya miezi miwili kukamilika ambapo amehoji kama zoezi hilo linaweza kufanyika kwa tanzania nzima ndani ya kipindi kifupi ili kufanyika kwa zoezi la upigaji kura ambao umepangwa kufanyika tarehe 30 mwezi wan ne mwaka huu.
Aidha amesema kuwa kutokana na upungufu huo unaoonekana kuielemea serikali na kushindwa kuweka wazi kwa watanzania kama zoezi hilo limeshindikana,JUKATA wanaitaka serikali kuacha mara moja kuilazimisha tume ta uchaguzi kuendesha zoezi la kura ya maoni kwa njia yoyote kwani hata mwenyekiti wa tume hiyo amekiri wazi kuwa zoezi hili litakuwa ngumu kufanyika kwa muda uliopangwa.
Mwanashiria wa JIKATA Bi GERINI FUKO akizngumzia kisheria juu ya mchakato huo ambapo amesema kuwa katika kuelekea mchakato huo wa upigaji wa kura ya maoni ili kupata katiba mpya imebainika kuwa sheria ya kura ya maoni ina mapungufu makubwa ambayo yanaweza kusababisha upigaji kura ya maoni ukaingia doa.
Amesema kuwa JUKATA wanaona hakuna umuhimu wala ulazima wa kulazimisha kupatikana kwa katiba mpya kwa sasa na badala yake serikali ihamishie nguvu zake katika uchaguzi mkuu wa Tanzania wa mwezi wa kumi kwani ni uchaguzi wa kihistoria na unahitaji maandalizi ya kutosha kwa wananchi ikiwemo utoaji wa elimu ya uraia kwa wananchi ili wawezi kuwachagua viongozi ambao watawasaidia kwa miaka mingine mitano.
Wanahabari mbalimbali kutoka Tanzania wakisikiliza kwa makini
Katika hatua nyingine JUKATA wamesema kuwa kama serikali itakuwa kiziwi na kiuendelea na kura ya maoni kwa kutumia daftari la zamani na hatimaye kupata katiba mpya wao wataanza mara moja harakati za kuwashawishi wananchi kuingia mitaani kuanza upya kudai katiba mpya nyingine kwani itakayopatikana itakuwa sio katiba kwa ajili ya watanzania wote.

No comments: