Tuesday, March 31, 2015

KIPAJI CHAKO AJIRA YAKO KIJANA,DC MAKONDA AJA NA HII NJEMA KWA VIJANA SASA,USIPITWE

Mkuu wa wilaya ya kinondoni DC PAUL MAKONDA akizngumza nna wanahabari mapema leo juu ya mchakato wa kusaka vipanji kinondoni ambao unatarajiwa kuanza hivi karibuni
 Mnamo tarehe 31 March mkuu wa wilaya ya Kinondoni, Paul Makonda amehitisha waandishi wa habari na kutangaza kuwa ameanzisha Kinondoni Talent Search ambayo itahusika kusaka vipaji vya watoto wenye vipaji kama; Kucheza, Kuimba, Kuchekesha na vingineo.
Akizungumza na waandishi wa leo alisema; Kinondoni Talent Search ni mpango wenye lengo kuu la kuwatambua vijana waishio kwenye wilaya ya Kinondoni wenye vipaji vya kuimba, Kuchekesha ambao wengi wao wapo katika mazingira magumu ya kiuchumi jambo linalowafanya kushindwa kuonesha vipaji vyao mwisho ndoto zao kufifia.Hivyo, lengo kuu la mpango huu ni kuwawezesha kupata njia za kutimiza ndoto zao kupitia uwezo wao
Mwimbaji maarufu ambaye ni mmoja kti ya wanakamati wa mashindano hayo PETER MSECHU mzaa wa SOPHIA REMIX akizngumza na wanahabari leo
 Kwa ufupi ni kwamba, Kinondoni Talennt Search inalenga kwanza, kuwatengeneza nafasi za mafanikio vijana wenye vipaji, kuwapatia mafunzo na kuwaunganisha na wadau muhimu waliopo kwenye sekta zao.Lakini kubwa zaidi, kutoa hamasa kwa vijana wote wa Wilaya ya Kinondoni na Tanzania kwa ujumla juu ya umuhimu wa kuendeleza vipaji vyao, kuepuka mambo yanayoweza kuviua na kuharibu malengo yao ya baadae, mfano matumizi ya dawa ya kulevya, ngono zembe na vitendo vya uporaji.Bila kusahau kuwakumbusha vijana wote kuwa ukimiliki kipaji unakuwa ajira, ni kujua tu namna ya kukitumia ili kikufae na kukufikisha utakapo, na ndio maana kauli mbiu ya mpango huu nikipaji chako, ajira yako’ alisema.
Msanii wa vichekesho mc PILIPILI naye alikuwepo
Ili kuhakikisha mradi huo unafanikiwa kwa kiwango cha juu na kufikia lengo, Paul Makonda ametengeneza kamati maalumu yenye wajumbe kutoka ofisi ya Mkuu wa wilaya pamoja na baadhi ya wasanii ambao wana uzoefu zaidi katika nyanja ambazo tunazigusa kwenye mpango huu.

1.Jumanne Mrimmy – Afisa utamaduni (Manispaa ya Kinondoni)
2.Sebastian Mhowera – Afisa Uhusiano – (Manispaa ya Kinondoni)
3.Peter Msechu – Msanii wa Bongo Fleva
4.Jokate Mwegelo – Mwimbaji/Mbunifu
5.Mc-pilipili -Mchekeshaji


No comments: