Friday, March 27, 2015

KUMBE ACT ZIKO MBILI TANZANIA,PINGAMIZI LATUA KWA MSAJILI TENA,TIZAMA HII

Baraza la Kilimo Tanzania (ACT) limekitaka chama cha siasa cha ACT – Tanzania kutotumia jina hilo kwa kuwa tayari baraza hilo limekwsha sajili jina la ACT kama kifupi cha jina la Baraza hilo.

Akizungumza leo katika kipindi cha television moja nchini tanzania kinachoruk siku , Mwenyekiti wa Baraza hilo Dkt Sinare Yusuf Sinare amesema kuwa jina ACT linatambulika kama kifupi cha Agricultural Council of Tanzania na kwa mujibu wa taratibu za hati miliki, jina hilo (ACT) halitakiwi kutumika na watu wengine hata kama litaambatanishwa na maneno mengine.
“Hata kama wakiongeza maneno, bado kuna ACT, hiyo ni nembo yetu, tumekwisha andika barua kwenda kwa msajili wa vyama vya siasa, pia tumeandika barua kwenda katika chama hicho lakini bado hatujapata majibu, nimekwisha ongea na Zitto Kabwe kuhusu hilo na kumweleza kuwa wanatakiwa kurekebisha kabla hatujaenda hatua za juu zaidi(Mahakamani) ambazo ni ghali.” Amesema Dkt Sinare



No comments: