Thursday, March 26, 2015

KUTOKA DAR ES SALAAM LEO--CUF WAMPA ONYO KALI RAIS KIKWETE,SOMA WALICHOKIZUNGUMZA LEO


Naibu mkurugenzi wa habari na uenezi wa chama hicho ABDUAL KAMBAYA akizngumza na wanahabari mapema leo jijini Dar es salaam kuhusu mchakato mzima wa uandikishwaji wa daftari la kudumu la wapiga kura katika mfumo wa kielecronic wa BVR
 Chama cha wananchi CUF leo kimemtaka Raisi wa jamhuri ya muungano wa Tanzania Dk JAKAYA KIKWETE pamoja na tume ya uchaguzi nchini kukiri mbele ya wananchi kuwa hakuna uwezekano wa kufanyika kwa kura ya maoni juu ya katiba pendekezwa kwa kile wanachodai ni kushindwa kukamilisha uandikishwaji wa daftari la kudumu la wapiga kura kwa wakati.
Akizungumza na wanahabari leo makao makuu ya chama hicho jijini Dar es salaam naibu mkurugenzi wa habari na uenezi wa chama hicho ABDUAL KAMBAYA amesema kuwa CUF wanaitaka tume ya taifa ya uchaguzi itamke kushindwa na kutokuwepo kwa uwezekano wa kuwepo kwa kura ya maoni ili kuepusha taifa kuingia gharama za kutumia fedha nyingi kuandaa kura ya maoni wakati zoezi lenyewe linaweza lisiwepo kwani ukamilifu wa uandikishwaji wa daftari la kudumu kwa mfumo wa BVR hauwezekani tena kwa tarehe iliyopangwa.
Amesema kuwa mbali na mazingira halisi ambayo yanaonyesha kuwa zoezi hilo limekwama na halitawezekana serikali imekuwa ikilazimisha kwamba inawezekana akitolea mfano kauli ya waziri mkuu aliyoitoa kuwa kura ya maoni iko pale pale na uandikishwaji utamalizika kwa wakati,hali ambayo amesema kuwa inaashiria hali isiyo njema kwa serikali ya CCM kuhusu hatma ya usala wa nchi wakati wa zoezi la kura ya maoni.

Amesema kuwa kuna mambo kadhaa ambayo yanafanya zoezi la BVR lisikamilike ikiwemo idadi kubwa ya watu wanaojitokeza ukilinganisha na vifaa husika,uwezo mdogo wa mashine hizo kufanya kazi,idadi ndogo ya madhine hizo,pamoja na serikali kutokuwa na hela ya kutosha kuendesha zoezi hilo kwa sasa,ambapo amesma kuwa hakuna muujiza wowote unaoweza kutokea katika zoezi hilo.
Akizungumzia kauli aliyoitoa Raisi KIKWETE na kunukuliwa na baadhi ya vyombo vya habari akivitaka vyombo vya ulinzi na usalama ikiwemo polisi kujiandaa kwa ajili ya zoezi la kura ya maoni,amsemaji huyo wa CUF amesema kuwa kauli hiyo ni kauli ya vitisho na kuashiria utawala wa mabavu na kusema kuwa huu sio muda wa mabavu ni muda wa kutafakari na kufanya maamuzi sahihi ambayo yatakuwa na manufaa kwa watanzania wote.
SOMA TAMKO NZIMA HAPO CHINI




No comments: