Saturday, March 28, 2015

PICHA --MPYA--ZITTO SIO MWENYEKITI ILA NI MKUU NA KIONGOZI,NA MSEMAJI MKUU WA CHAMA,ACHAGULIWA RASMI

Kiongozi mpya wa chama cha ACT Tanzania Zitto Kabwe, akilakiwa na wajumbe wa mkutano mkuu wa chama hicho, wakati wa uchaguzi mkuu uliofanyika kwenye ukumbi wa Kadinali Rugambwa, Oysterbay jijini Dar es Salaam, Jumamosi Machi 28, 2015. 

Zitto alichaguliwa kuwa kiongozi wa chama hicho nafasi ambayo kwa katiba ya chama hicho ndiyo ya juu zaidi. Nafasi zingine ni Mwenyekiti wa chama, namakamu wake, wa Tanzania visiwani na Tanzania bara, hali kadhalika nafasi ya ukatibu mkuu na manaibu wake wiwili. 

Chama hicho kitazinduliwa rasmi Jumapili kwenye ukumbi wa Diamond Jubilee Hall jijini Dar es Salaam.

hawa ni wajumbe wa NEC waliochaguliwa 
Zanzibar
Halima M Hamis
Said Ismail
Rashid S Ali
Juma Said Saanane 
Halua Ali Amali
Tanzania Bara
Marunga Msimba
Ali Mwinyi 
Sophia Yamola
Fungo G Benson
Charles Lubala
Godfrey Sanga 
Likapo B Likapo
Batulo Ibrahim 
Kirungi A Kirungi 
Alex Nsanga


No comments: