SIKILIZA SAUTI HII,GWAJIMA AOMBA MSAMAHA,ASISITIZA PENGO ALIKOSEA

ASKOFU JOSEPHAT GWAJIMA AJISALIMISHA POLISI KWA MKUU WA UPELELEZI KANDA MAALUM DAR ES SALAAM
Jeshi la Polisi Kanda Maalum Dar es Salaam limeanza kumhoji Askofu JOSEPHAT GWAJIMA wa Kanisa la Ufufuo na Uzima baada ya kujisalimisha kama alivyotakiwa kufanya hivyo na Kamishana wa Polisi Kanda Maalum ya Dar es Salaam.

Askofu Gwajima alifika kituo kikuu cha Polisi saa nane na dakika kumi na tano mchana wa tarehe 27/03/2015. Mara baada ya kufika kituoni hapo alielekezwa kwenda kumuona Mkuu wa Upelelezi wa Kanda Maalum ya Dar es Salaam SACP Constantine Masawe ambaye alikuwa akisubiri kufika kwake.

Tuhuma zinazomkabili Askofu Gwajima ni pamoja na kumkashfu na kumtukana hadharani Kiongozi wa Kanisa Katoliki Jimbo Kuu la Dar es Salaam Mwadhama Polycarp Kardinali Pengo

Taratibu za mahojiano zimekwishaanza kwa mujibu wa sheria na mtuhumiwa atapewa haki zote anazostahili kama vile kuwa na ndugu yake wa karibu, rafiki yake anayemwamini au wakili wake.
Kama ilivyo kawaida utakusanywa ushahidi kutoka pande zote za shauri hilo ili kubaini ukweli wa jinsi tukio hilo lilivyotokea na athari zake.

Baada ya hapo hatua nyingine za kisheria zitachukuliwa ikiwa ni pamoja na kupata maoni ya kitaalamu na ya kisheria ili kuhakikisha kwamba haki inatendeka. Ili ufanisi upatikane katika upelelezi wa shauri hili, ni muhimu kupata ushirikiano kutoka kwa kila atakayetakiwa kulisaidia Jeshi la Polisi kukamilisha haraka upelelezi wa shauri hili ambalo sasa limepata mvuto mkubwa katika jamii.


HAPA SAUTI YAKE AKIZUNGUZIA KILICHOTOKEA 

About HABARI24 TV

Post a Comment
Powered by Blogger.