Monday, March 9, 2015

SOMA NA USIKILIZE JINSI DK SLAA ANGEUAWA KIRAHISI NA MLINZI WAKE,MABERE MARANDO ASIMULIA MKANDA MZIMA

 Sikiliza Audio Ya Taarifa Kuhusiana na Mkakati unaodaiwa kuandaliwa na CCM wa kumuua Dk. Slaa wavuja
MABERE Marando- Mjumbe wa Kamati Kuu ya Chamacha Demokrasia na 
Madendeleo (Chadema), amefichua mawasiliano ya siri yanayofanywa na 
vyombo vya dola dhidi ya chama, na mkakati wa kumdhuru Katibu Mkuu, Dk. 
Willibroad Slaa.

Amesema kuwa Idara ya Usalama wa Taifa na Makamu 


Mwenyekiti wa CCM 
Taifa, Philip Mangula, wamekuwa wakimtumia Khalid Kagenzi-mlinzi binafsi
wa Dk. Slaa ili kurekodi na kuvujisha taarifa za vikao vya siri vya 
Chadema.


“Kama chama tumelalamikia sana serikali ya CCM kwa matumizi mabaya ya 
vyombo vya dola dhidi yetu. Sasa tumebaini wanatumia vijana wetu kunasa 
taarifa zetu.

“Kagenzi kwa miaka miwili tumebaini amekuwa akitumika kupeleka taarifa 
za Chadema kwa usalama wa taifa. Amekiri hilo kwa maandishi na kutaja 
namba za watu wa usalama anaowasiliana nao,” amesema.

Marado alimtuhumu Mangula kuwa imebainika anawasiliana na Kagenzi ikiwa 
ni pamoja na kumtumia fedha mara mbili, Julai 24 na Desemba 4 mwaka 
jana, kupitia simu yake ya Vodacom (anaitaja).

Kwa mujibu wa Marandu, mlinzi huyo alipobanwa zaidi alieleza mkakati 
uliokuwa ukipangwa na watu hao wa kumwekea Dk. Slaa sumu kwenye chakula 
au kinywaji.

Amesema kuwa wamebaini nyendo hizo hivi karibuni baada ya mlinzi huyo 
kuonekana akipanda katika gari ya afisa usalama wa mkoa wa Kinondoni 
lenye namba za usajili T213 ARS, akiwa nalo afisa msaidizi.

Marando amefafanua kuwa watamfikisha Kagenzi polisi ili achunguzwe na 
hatua zaidi zichukulie, lakini akakataa kuweka hadharani namba za simu 
na majina ya maafisa usalama aliodai wako zaidi ya 22.

Amesema kuwa pia wamenasa taarifa za maofisa hao za kumtumia Kagenzi 
muda wa maongezi zaidi ya shilinigi milioni saba kwa nyakati tofauti.



No comments: