Friday, March 6, 2015

TAARIFA MUHIMU KWA WALE WENYE MALENGO YA KUPANDA TRENI KUANZIA LEO

Uongozi wa Kampuni ya Reli Tanzania – TRL umetangaza kusitishwa huduma za safari ya treni abiria kuanzia leo Ijumaa Machi 06, 2015 kufuatia eneo la tuta la reli kati ya stesheni za Kilosa na Kidette kuharibika kwa mafuriko ya mvua inayonyesha hivi  sasa katika eneo hilo.

Kwa mujibu wa taarifa hiyo Wahandisi na Mafundi wa TRL wako katika eneo la tukio wakifanya tathmini ya jinsi zoezi la ukarabati utakavyofanyika na kwa muda gani.

Ikifafanua zaidi taarifa imeeleza kuwa tathmini ya mafundi hao ndiyo itakayoamua huduma hiyo ya usafiri wa treni za abiria  itarejea lini.


Imetolewa na Afisi ya Uhusiano ya kwa niaba ya 

Mhandisi Kipallo Aman Kisamfu 

Mkurugenzi Mtendaji –TRL

Dar es Salaam

Machi 06, 2015 

No comments: