Monday, April 6, 2015

MATOKEO YA SIMBA NA KAGERA SUGAR YAKO HAPA




Timu ya Simba SC klabu imeibamiza bao 2-1 timu ya Kagera Sugar katika mchezo wa ligi kuu Vodacom Tanzania bara uliofanyika katika uwanja wa CCM Kambarage mjini Shinyanga.

Mtanange huo ulitarajia kufanyika siku ya Jumamosi iliyopita lakini kutokana na hali ya hewa kuwa mbaya baada ya maji kujaa uwanjani mchezo uliahirishwa.

Simba SC imejipatia bao la kwanza kipindi cha pili katika dakika ya 52 kupitia kwa mchezaji wake Ramadhani Singano,dakika ya 64 Kagera Sugar wakasawazisha bao kupitia kwa mchezaji wake Rashid Mandawa lakini dakika ya 71 Emmanuel Okwi akaipatia Simba bao la pili kwa njia ya penati.

Mchezo umeisha Kagera Sugar wanaonesha kutoridhika na matokeo vurugu za aina yake zimejitokeza lakini hali imetulia

No comments: