Friday, April 10, 2015

MBOWE JANA KAFANYA JAMBO LINGINE HUKO HAI-TIZAMA HAPA




MWENYEKITI wa kambi ya upinzani Bungeni ambaye ni Mbunge wa Hai Freeman Haikaeli Mbowe leo ametimiza ahadi aliyo waahidi Wananchi wa Jimbo lake la Hai kwa kuwapatia magari mawili ya kubebea wagonjwa.
Mbowe amesema kuwa magari hayo yatafanya kazi pasipo kuwa na itikadi za chama kwani wananchi wote ni wamoja hasa katika shughuli za kuleta maendeleo.
Amebainisha kuwa gari moja lita tumika katika Hosipitali ya Wilaya ya Hai na gari lingine lita tumika kutoa huduma katika hosipitali Machame ambayo inamilikiwa na kanisa la Kiinjili la Kilutheri Tanzania.

Zifuatazo ni picha tofauti za tukio la kukabidhi magari hayo katika mkutano ulio fanyika Wilayani Hai eneo la Snoview Hotel.



Mbunge Freeman Mbowe akiwasili katika viwanja vya Snowview 




Magari ya kubebea wagonjwa (ambulance)zikiwasili uwanjani 






Mbunge Freeman Mbowe akiwa uwanjani hapo na kuonesha upendo kwa kumbeba Mtoto






Sehemu ya ndani ya gari la kwanza la kubebea wagonjwa. 



Sehemu ya ndani ya gari la pili la kubebea wagonjwa. 





Upande wa nyuma wa magari hayo kama unavyo someka. 



Mbowe akikabidhi vitambulisho vya gari kwa Mkuu wa Jimbo la KKKT Jimbo la Hai
Mchungaji Asanterabi Swai



Mbowe akikabiti vitambulisho vya gari la kubebea wagonjwa kwa Mganga Mkuu wa
 Hosipitali ya Wilaya ya Hai Dr Paul Chaote aliye pokea kwa niaba ya Mkurugenzi Mtendaji.

 picha Zote na Devis Minja wa Pamojahabariblogspot.com

No comments: