Wednesday, April 15, 2015

MNYIKA ATOA KAULI NYINGINE MUDA HUU--ISIKUPITE HII MTANZANIA

Naibu katibu mkuu wa chama cha democrasia na maendeleo CHADEMA mh JOHN MNYIKA ameitaka serikali kuchukua hatua za maksudi na za haraka kukabiliana  na alilliita janga la kiataifa la ajali nchini badala ya kusubiri ajali itokee na kuishia kutoa pole kwa wafiwa bila kuchukua hatua za haraka kuzuia ajali hizo.

Akizungumza na wanahabari mapema leo mh JOHN MNYIKA ambaye ni mbunge wa ubungo amesema kuwa kwa hali ya ajali iliyofikiwa nchini na kulinganisha na takwimu zilizotolewa jana na kamanda wa polisi wa usalama barabarani inatosha kusema kuwa ajali nchini Tanzania ni janga la kitaifa na kuhakikisha zinachukuliwa hatua za dharura kukabiliana nazo.


Amesema kuwa hatua ambazo zilitangazwa na kamanda wa polisi wa usalama barabarani jana kuwa watahakikisha kuwa wanawafutia leseni madereva wote watakaobainika kusababisha ajali nchini bado sio hatua madhubuti za kukabiliana  na tatizo hilo na badala yake ni mwendelezo wa serikali kufanyia kazi matukio yanapotokea na kushindwa kuzuia chanzo cha matukio hayo.


Katika hatua nyingine mbunge huyo wa jimbo la ubungo kupitia CHADEMA ameitaka serikali kupitia tume ya taifa ya uchaguzi kutangaza ratiba ya uandikishwaji wa daftari la wapiga kura kwa mfumo wa BVR kwa mikoa yote ambayo bado zoezi hilo halijafanyika kutokana na kile alichokiita ni kupigwa danadana kwa zoezi hilo huku dalili zikionyesha kuwa kuna uwezekano lisifanikiwe kwa asilimia kubwa hata kama vifaa vyote vilivyoagizwa vitawasili nchini.

No comments: