Saturday, April 11, 2015

RUSHWA YA NGONO BADO NI TATIZO KUBWA TANZANIA

Jaji mstaafu wa mahakama ya rufaa nchini tanzania mama EUSEBIA MUNUO  ambaye alikuwa ndiye mkufunzi katika mafunzo hayo yaliyoendeshwa leo jijini Dar es salaam
 Rushwa ya ngono pamoja na matumizi mabaya ya madaraka yametajwa kuwa ni moja kati ya matatizo makubwa ambayo yamezidi kuweka mizizi nchini tanzania na kuwaadhiri wasichana wengi huku sheria ikishindwa kuweka wazi adhabu mahususi ili kuwabana wanaohusika katika swala hilo.
Hayo yamesemwa leo jijini dare s salaam na Jaji mstaafu wa mahakama ya rufaa nchini tanzania mama EUSEBIA MUNUO wakati akiendesha mafunzo maalumu kwa wanafunzi wa chuo kikuu cha Dar es salaam mafunzo yaliyolenga kuzungumzia madhara na jinsi rushwa ya ngono inavyoathiri kizazi kukubwa cha wasichana wa sasa nchini tanzania.


Wanafunzi mbalimbali kutoka chuo kikuu Dar es salaam waliohudhuria katika mafunzo hayo leo jijini Dar es salaam
Amesema kuwa tatizo la ruswa ya ngono limekuwa likiongezeka siku hadi siku nchini kutokana na kutokuwa na sheria mahususi ambayo inawaadhibu moja kwa moja  wahusika katika swala hilo.
Amesema kuwa wasichana wengi wanapokuwa katika harakati za kutafuta ajira katika maofisi mbalimbali wamejikuta wakitumia miili yao kuwashawishi mabosi wao ili waweze kupata ajira jambo ambalo amesema kuwa sio sahihi na wasichana hao wamekuwa wakikosa msaada kuhusu swala hilo.
  Amesema kuwa hata katika maofisi mbalimbali kumekuwa na wasichana ambao hawana vigezo vya kuwa katika maofisi hayo ila wapo tu kwa sababu wanatembea na mabosi wao jambo ambalo limetajwa kuleta madhara makubwa ikiwemo kushusha ufanisi wa kazi pamoja na ofisi husika kwa ujumla.
Mwanafunzi CATHERIN OLOMY akizungumza na mwandishi wa mtandao huu juu ya mafanikio ya semina hiyo ya siku moja kwao na kwa jamii kwa ujumla
Baadhi ya wanafunzi ambao wamehuduria mafunzo hayo ya siku moja ambayo yameandaliwa na WLAC kwa kushirikiana na TAWLA mwanafunzi
CATHERINE OLOM
Y ambaye ni mmoja ya washiriki anasema kuwa  mafunzo hayo ni muhimu sana kwa wanafunzi wa sasa hususani wasichana kwa kuwa yatawasaidia kujiamini kujua haki zao kama wanafunzi na watoto wa kike,ikiwa ni pamoja na kujua uthamani wao pindi wanapokutana na swala la rushwa ya ngono.

No comments: