Thursday, April 9, 2015

SAMAHANI PICHA ZINATISHA--HII NI HUKO MOSHI MWIKA SOKONI LEO

Kama ulidhani matukio ya kuchoma watu moto pale wanapokamatwa na makosa hususani ya kiijambazi ni kwa baadhi ya maeneo unakosea sana,tukio hili limetokea leo mkoani kiilimanjaro katika jimbo la vunjo maeneo ya mwika sokoni ambapo majambazi wawili ambao walikua na silaha na kujaribu kupora lakini wananchi wenye hasira kali wakawashtukia na kuwatia mikononi na kilichofwata ni mauaji ya kutisha.


Mashughuda wa tukio hilo kutoka mwika sokoni ambao wamezungumza na mtandao huu wamedai kuwa majira ya asubuhi kiukaribia mchana majambazo wannne  walivamia eneo la maduka sokoni hapo karibu na stendi ya magari ya kwenda moshi na kufwetua risasi hewani hovyo hovyo bila mafanikio ndipo wananchi walifanikiwa kuwadhibiti majambazi lakini wawili walifanikiwa kuchomoka na kutoweka na ndipo jumba bovu lilipowaangukia vijana wawili na kukutana na unyama wa aiana yake.


Mashughuda wa tukio wanazidi kutuambia kuwa baada ya kusalia wawili wananchi waliamua kufanya ukatili wa aina yake baada ya kuamua kuwashushia kipigo cha mbwa mwizi na baadae kufanya unayama mkubwa wa kumwagia mafuta ya taa na kumvisha tairi na kisha kumchoma moto hali iliyoonyesha hasira za wananchi hao juu ya matukio ya ujambazi kama hayo maeneo hayo.

Habari zinasema hadi polisi wanafanikiwa kufika katika eneo la tukio kujaribu kuwatawanya wananchi hao na kumuokoa kijana huyo walikuta tayari ameshakuwa kama mkaa jambo ambali liliwafanya polisi kushindwa kufanya jambo zaidi ya kuchukua mwili wa kijana huo na kuondoka nao.


SAMAHANI PICHA ZA CHINI KAMA HUTAMANI KUZIONA USIENDELEE 








Mtandao huu bado unafwatilia kwa ukaribu muendelezo wa tukio hili

No comments: