Tuesday, April 28, 2015

WAZIRI MWAKYEMBE AKUTANA NA TAFFA OFISINI KWAKE,AWAAHIDI KUWAKUTANISHA KWA PAMOJA HIVI KARIBUNI

 Waziri wa ushirikiano wa Africa mashariki mh HARISON MWAKYEMBE amekutana Uongozi wa wakala wa  forodha na uondoshaji shehena Tanzania(TAFFA),kwa lengo la kukaa kwa pamoja na kujadili chamgamoto mbalimbali ambazo zinaikabili secta hiyo katika nchi za Africa mashariki.

Akizungumza katika ,mkutano huo waziri mwakyembe amesema kuwa ameamua kukutana na wakala  hao kutokana na mchango mkubwa walionao katika kuinua uchumi wa nchi na amekuwa na mahusiano ya karibu na wakala hao tangu akiwa waziri wa uchukuzi hadi sasa wizara ya Africa mashariki.
Waziri mwakyembe amesema kuwa amekuwa akipokea kero nyingi za maswala ya uondoshwaji wa shehena kutoka katika nchi za Africa mashariki na kuzitatua lakini ameshangaa kwanini Tanzania wamekuwa wagumu kupeleka kero zao kwa waziri huyo jambo ambalo limemsukuma kukutana na wadau kama hao ili kujua ni changamoto gani zinawakabili na jinsi gani wanaweza kuzitatua kwa pamoja.
Waziri wa ushirikiano wa africa mashariki mh HARSON MWAKYEMBE akizngumza na Uongozi wa wakala wa  forodha na uondoshaji shehena Tanzania(TAFFA) alipokutana nao ofisini kwake jana kwa lengo la kubadilishana mawazo na kujua changamoto mbalimbali ambazo zinawakabili katika shughuli zao
Wakizungumza na waziri huyo viongozi wa TAFFA wameonyesha kutokuwa na imani na mamlaka ya mapato Tanzania TRA kwa kile walichokiita ukiritimba uliokithiri juu yao wanaofanyiwa na mamlaka  hayo ikiwemo dharau pamoja na kutosikilizwa keri zao jambo ambalo waziri MWAKYEMBE amesikitishwa nalo na kuahidi kulifanyia kazi mara moja


Aidha wakala hao wamelalamikia mfumo mbovu wa utoaji wa leseni kwa ajili ya kufanya kazi zao ambao kwa sasa leseni kwa wakala hao zimekuwa zikitolewa kwa mwaka mmoja jambo ambalo wamedai ni kero kwao kwani wamekuwa wakitumia muda mwingi sana katika kufwatilia leseni kuliko kufanya kazi za kampuni zao jambo ambalo pia waziri mwakyembe ameahidi kulisimamia kwa kina kuhakikishakuwa miaka ya leseni ya kazi zao inaongezwa ili kuwapa unafuu wao katika kufanya kazi zao.

Katika mkutano huo baada ya kuonekana wazi kuwa wakala hao wana changamoto nyingi za kuzungumza waziri MWAKYEMBE aliahirisha mkutano huo na kuahidi kuwakutanisha tena siku za karibuni kujadili kwa kina changamoto zinazowakabili ambapo mkutano huo unatarajiwa kujumuisha wadau wengine wengi akiwemo waziri wa fedha pamoja na wadau kutoka mamlaka ya mapato Tanzania TRA.


No comments: