Monday, May 25, 2015

BANG MAGAZINE WAAZIMISHA MIAKA 11 YAO KWA MAFANIKIO MAKUBWA

Mkurugenzi wa BANG! Emelda Mwamanga akionyesha toleo jipya la sasa ambalo limeelezea maisha halisi ya waziri wa maliasili na utalii mh LAZARO NYALANDU.wakati akizngumza na wanahabari leo jijini Dar es salaam

 Jarida maarufu nchini Tanzania na Africa mashariki jarida la BANG leo limeazimisha miaka 11 tangu kuanzishwa kwake kwa huku wakijivunia mafanikio makubwa ya kuwafikia watanzania wengi.


Akizungumza na wanahabari leo mapema jijini Dare s salaam katika hafla fupi ya kuazimisha miaka hiyo nya kuzaliwa kwa jarida hilo Mkurugenzi wa BANG! Emelda Mwamanga amesema kuwa uongozi wa gazeti hilo umejipanga kuhakikisha kuwa unaendelea kuwasaidia wanawake wa kitanzania katika kuwanyanyua kiuwezo kama ambapo malengi ya gazeti hilo ambalo lilianzisha mahususi kwa ajili ya kuwasaidia wanawake.

Kuhusu lugha inayotumika na gazeti hilo ambayo ni ya Kiingereza amesema kuwa sasa jarida hilo limeamua kutoa jarida linguine kwa ajili ya wasomaji wa lugha ya Kiswahili kwa lengo la kuwafikia watanzania wote kwa ujumla wao.





Miaka kumi na moja ya jarida la BANG!

Naomba nianze kwa kumshukuru mwenyezi mungu mwingi warehema kwa kutujalia uzima na kutuwezesha kutukutanisha leo.
Ndugu waandishi wahabari napenda kutumia fursa hii kuwashukuru tena kwa kuitikia wito wetu na kuhudhuria mkutano huu muhimu ambao dhumuni lake kubwani kuelezea jarida letu la BANG!  Lilivyojipanga kuinua na kukuza vipaji vya wanawake nchini katika miaka ijayo.

Jarida la BANG! Katika kipindi chote tangu kuanzishwa kwake limekuwa likiandika habari mbalimbali kuhusiana na masuala ya wanawake, vijana na jamii na kuwezesha kuwainua vijana kwa kuvitambulisha vipaji vyao.

Katika kusherehekea miaka kumi na moja jarida letu limejipanga kuhakikisha linajikita zaidi kuinua maisha ya wanawake kwa kuvitambulisha vipaji na biashara zao na kuandika habari mbalimbali zitakazowawezesha kutambulika Afrika yote kwa ujumla. 

Jarida la BANG! Limekuwa likisambazwa katika mikoa yote ya Tanzania,  Kenya na Uganda.  Moja ya mipango mikubwa tunayoiandaa ni kuweza kulisambaza jarida la BANG! Katika nchi ya Rwanda, Burundi, Malawi na Zambia katika kipindi kisichozidi miaka miwili ijayo.

Katika kusherehekea miaka kumi na moja jarida letu pia limekuwa likitambua michango mbalimbali iliyoletwa na viongozi wetu wa kisiasa katika majimbo yao na kutaka katika kipindi hiki cha  kuelekea uchaguzi mkuu jamii iweze kuwatambua viongozi wanaowachagua kwa kuyafahamu maisha yao.

Leo tunasheherekea miaka 11 ya Jarida letu lenye mafanikio makubwa kwenye kazi zetu tukaona ni vyema kumshirikisha Mheshimiwa Waziri Lazaro Nyalandu na Mkewe Faraja Nyalandu kwenye toleo hili maalum kuelezea historia ya maisha yao.

“ Tunawakaribisha viongozi wote wakisiasa kuonesha ushirikiano wao kwa kuwa wazi kuelezea yote waliyoyafanya katika majimbo yao na kuelezea maisha halisi ya familia zao ilijamii iweze kuwatambua zaidi.”

Pia jarida letu linawashukuru wadau wote ambao kwanamna moja ama nyingine wametuwezesha kufika miaka 11 ya usambazaji wajarida letu la BANG!
Kwa kuwezesha yote hayo jarida letu limeboresha zaidi kazi zake kwa kuzifanya ziwe na ubora unaokubalika kimataifa, hivyo ilikufanikisha hayo limepandisha gharama zake ilikuweza kufanikisha hayo yote.

Katika kusherehekea miaka 11 tunapenda kuwashukuru wadau wote wakiwemo viongozi waserikali pamoja na wadau wengine kwa ushirikiano wao wanaouonesha kwa jarida hili na kuliwezesha kufika mbali.

Lengo kubwa la jarida hili ni kuhakikisha kazi za wanawake wakitanzania zinatambulika Afrika yote ilikuwawezesha kuinua uchumi wao kupitia kuibua vipaji vyao kwa kuziandi kakazi zao iliwaweze kutambulika
Asante ni kwa kunisikiliza.

Mkurugenzi wa BANG! Emelda Mwamanga.

MWISHO

No comments: