Mkutano wa 20 wa bunge la bajeti ambao ni mkutano wa mwisho wa bunge hilo kuelekea uchaguzi mkuu wa mwaka huu umeanza leo mjini Dodoma hadi june 27 ikiwa ni siku 44 za mwisho wa bunge hilo.
Mkurugenzi wa habari Elimu kwa umma na uhusiano wa kimataifa Bw. Josey Mwakasyuka bajeti ya Wizara ya Waziri mkuu imepangwa kwa siku tano kutokana na mabadiliko ya ratiba ya bunge hilo.
Amesema bunge hilo la bajeti ambalo kawaida huanza mwezi april lilisogezwa mbele hadi leo kutokana na ratiba ya awali ya Tume ya Taifa ya uchaguzi NEC, kupanga kufanyika kwa kura ya maoni ya Katiba inayopendekezwa na zoezi hilo likaahirishwa.
Mwakasyuka amesema bajeti kuu ya serikali itawasilishwa juni 11 mwaka huu sambamba na nchi zingine za jumuiya ya Afrika mashariki
No comments:
Post a Comment