Chama cha wananchi CUF
kimesema kuwa ipo hatari ya asilimia kubwa ya watanzania kukosa haki yao ya
msingi ya kupiga kura kutokana na wananchi wengi kushindwa kujiandikisha katika
daftari hilo kwa sababu ya muda wa kujiandikisha katika zoezi husika
kumalizika.
Hayo yamesemwa leo
jijini Dar es salaam na mwenyekiti wa chama hicho profesa IBRAHIM HAROUNA
LIPUMBA wakati akizungumza na wanahabari kuhusu ziara ya kukagua zoezi hilo
iliyofanywa na viongozi wakuu wa chama hicho katika mikoa ambayo zoezi hilo
linaendeshwa kwa sasa.
Amesema kuwa katika
tathmini waliyofanya wamegundua kasoro nyingi ikiwemo wananchi kutokuwa na
taarifa za zoezi hilo katika maeneo yao,uandikishwaji kusua sua kwa siku za
mwanzo kutokana na wahusika kutokuwa na uzoefu na mashine zinazotumika,hivyo
katika maeneo mengi siku saba ambazo ndio zinatumika kuandikisha katika eneo
moja hazikutosha hivyo kuna idadi kubwa ya watanzania wamekosa haki hiyo ya
kujiandikisha.
Mh LIPUMBA akitolea
mfano katika kijiji cha milonde,kata ya matemanga,wilaya ya tunduru asilimia 60
wenye haki ya kuwa wapiga kura hawakupata nafasi ya kuandikishwa katika daftari
hilo nkwa kigezo cha siku saba kumalizika hivyo mashine za BVR zimehamishwa
ambapo katika idadi ya wapiga kura 2260 waliandikishwa ni 920 tu ambapo tatizo
hilo limeonekana katika vituo vingi huku akisema kuwa hali hiyo ni hatari kwani
watanzania wengti watakosa haki ya kupiga kura.
Amesema kuwa kutokana
na hali hiyo chama cha wananchi CUF kinaiomba serikali kuongeza siku za uandikishwaji
kutoka siku saba za sasa hadi kufikia siku 14 kama tume ya uchaguzi
ilivyotangaza mwezi wa julai 2014.
Ameongeza kuwa serikali
lazima iipe tume ya uchaguzi fedha za kutosha kukamilisha zoezi la kuandikishwa
wapiga kura pamoja na serikali kupunguza kupoteza pesa nyingi katika maandalizi
ya kura ya maoni na katiba inayopendekezwa kwani kisheria kura hiyo haiwezi
kufanyika kwani sheria ya kura ya maoni
imeshavunjwa na hivi sasa hakuna sheria inayoweza kusimamia kura ya maoni.
No comments:
Post a Comment