Tigo, kampuni
yenye ubunifu zaidi wa kidijitali nchini na EduMe, inayotoa huduma ya kwanza ya kimataifa ya mambo ya elimu kupitia simu
wamezindua bidhaa ya kipekee ya ujasiriamali kwenye simu kwa wateja wa Tigo nchini
Tanzania.
Shule ya Biashara inawawezesha
watumiaji kujifunza ujuzi wa biashara na ujasiriamali kwa bei nafuu kabisa kupitia kwenye simu yoyote ya mkononi. Tigo Tanzania,
ambayo ni sehemu yakampuni yakimataifa ya mawasiliano ya simu
na vyombo vya habari ya Millicom, ni ya kwanza barani Afrika kuzindua huduma kama hii.
Kwa mujibu wa Mkuu wa kitengo
cha kidijitali Bw. Yaya N 'Djore alisema"
Kampuni ya Tigo Tanzania ilituzwa ruzuku YA ubunifu kutoka GSMA Connected Women
ilikutengene za huduma ya "Shule ya Biashara” mafunzo ya ujasiriamali wa kwenye simu yanayolenga kuwaandaa wajasiriamali wenye
kipato kidogo kuwa na ujuzi unaohitajika kuanza au kukuza biashara "
Somo linatumia hadithi za
wamiliki wabiashara wandani na masomo yaliyo chambuliwa ilikutoa mwongozo kwa watumiaji
kupitia kila hatua muhimu ya kuanzisha na kuendesha biashara. Masomo yanaelezea
mada kama vile, jinsi ya kuchagua wazo la kibiashara, jinsi ya kuongeza uelewa kuhusu
biashara na jinsi ya kusimamia biashara yako. Masomo yanatolewa kwa njia ya ujumbe
mfupi au sauti kwa lugha ya Kiswahili na kufanya yapatikane kwenye simu yoyote,
na kwa watu wenye uelewa mdogo wa lugha ya kiingerezana au ngazi ya elimu. Baada ya kukamilisha masomo
watumiaji wanaweza kupata vyeti vya ujasiriamali vya EduMe-Tigo.
Pia watapata fursa ya kuomba
mikopo midogo kupitia kwenye ushirikiano wa Tigo na Benki ya Afrika na Benki ya
Wanawake ya Covenant (Tanzania) Ltd.
Meneja Mkuu wa Tigo
Tanzania Bw. Diego Gutierrez, alisema: "Tumefurahi kutoa huduma hii kubwa na
mpya kwa wateja wetu. Kuna mahita ji makubwa ya elimu ya biashara nchini
Tanzania kwasababu wajasiriamali ndio wanaounda uti wa mgongo wa uchumi wa
Tanzania. Kampuni ya Tigo inadhamira ya kukuza maisha ya kidijitali na kubadilisha
maisha. Elimu ni muhimu katika hili."
Mkurugenzi Mtendaji wa EduMe
Bw.Jacob Waern, alielezea: "Tumefurahi kutoa fursa kwa mamilioni ya watu nchini
Tanzania kupata mafanikio katika biashara zao. Dhamira yetu ni kuanzisha huduma
mpya za simu zinazohusu elimu ambazo zitawawezesha wateja wetu kujifunza kwa wakati
wowote na mahali popote.
Kutokana na kujikita kwao
kwenye ubunifu katika masoko ya ndani na dhamira yao ya kutoa huduma tofauti kwa
wateja, Kampuni ya Tigo ni mwenza sahihi wa EduMe."
Huduma ya Shule ya Biashara
inapatikana kwa wateja wa Tigo. Wateja wanaweza kupata huduma hii kwa kupiga *
148 * 33 # au kwa kutuma ujumbe wenye neon Biashara kwenda 15633.
Ingawa huduma ilifunguliwa
kwa watumiaji wachache mwezi Oktoba 2014, huduma mpya ambayo nirahisi kwa watumiaji
sasa inapatikana kwa wateja wote wa Tigo. Hadi sasa, Shule ya Biashara ya Tigo imetoa
zaidi ya masomo 100,000.Zaidi ya watumiaji 11,000 wameshatumia huduma hii, kati
ya hao watumiaji 4,000 niwanawake.
No comments:
Post a Comment