Friday, May 22, 2015

HII NI SHULE-IPO CHALINZE.ITIZAME HAPA

Na John Gagarini, Globu ya Jamii - Chalinze

WANANCHI wa Kijiji cha Mkoko wilayani Bagamoyo mkoani Pwani wameiomba Halmashauri kubomoa baadhi ya madarasa ya shule ya Msingi Mkoko ambayo yananyufa na yako hatarini kuanguka hivyo kufanya wanafunzi kusoma kwa hofu.

Akizungumza kwenye mkutano wa hadhara uliofanyika kijijini hapo hivi karibuni Muhsin Mkumbi alisema kuwa majengo hayo yako kwenye hali mbaya na wakati wowote yanaweza kuanguka na kuleta madhara.


Mkumbi alisema kuwa madarasa hayo ni mabovu sana na hayastahili kutumika kutokana na ubovu wake hivyo ni vema Halmashauri ikayabomoa na kuyajenga upya ili kuepuka madhara ambayo yanaweza kutokea.
"Madarasa hayo yameharibika sana na yataanguka wakati wowote hivyo tunaiomba halmashauri iyabomoe kwani ni hatari kwa wanafunzi na walimu wanaofundisha shule hiyo, hali ni mbaya sana tunaomba hatua madhubuti zichukuliwe," alisema Mkumbi.

Alisema kuwa hata baadhi ya wanafunzi wamekuwa wakiogopa kwenda shule kutokana na hali hiyo ya ubovu wa madarasa hayo ambayo yamewekewa na miti kuyazuia ili yasianguke na tunawasiwasi kwani yakianguka yataleta tatizo.

Kwa upande wake ofisa elimu wa kata ya Msata Rajab Msakam alikiri kuwepo kwa tatizo hilo na kusema kuwa madarasa mengi yana nyufa kutokana na ardhi ya eneo hilo ujenzi wake kuwa mgumu kwani inapasuka na kusababisha nyufa.

Msakamali alisema kuwa talipeleka jambo hilo sehemu husika ili kuangalia namna ya kuikabili hali hiyo ambayo inahatarisha usalama wa wanafunzi pamoja na walimu wanaofundisha madarasa hayo yenye nyufa.

Naye Mbunge wa Jimbo hilo Ridhiwani Kikwete alisema kuwa tayari suala hilo limepelekwa halmashauri na kinachosubiriwa ni kibali kwa Kijiji kwa ajili ya kuvunja madarasa hayo ambayo yanahatarisha usalama wa wanafunzi na walimu.(Muro

No comments: