IDADI
YA WALIOTHIBITISHWA KUFARIKI DUNIA KUTOKANA NA MAFURIKO JIJINI DAR ES SALAAM
YAFIKIA WATU KUMI NA MBILI
Watu
wapatao kumi na wawili wamethibitishwa kupoteza maisha jijini Dar es Salaam
kutokana na athari za mafuriko kufuatia mvua zinazoendelea kunyesha katika jiji
hilo. Idadi hii inatokana na taarifa ya awali ya Jeshi la Polisi kwa vyombo vya
habari iliyotaja idadi ya waliopoteza maisha kuwa ni wanane (08). Hili ni
ongezeko zaidi ya watu waanne (04). Watu walioripotiwa kuongezeka hadi sasa ni
kama ifuatavyo:
1.
Mnamo 09/05/2015 majira ya saa 12:00
katika bonde la mto Mkwajuni, mtaa wa Makuti, Magomeni wilaya ya Kinondoni,
ulipatikana mwili wa mtu mmoja mwanamke anayekadiriwa kuwa na umri kati ya
miaka 40 – 45 akiwa amefariki dunia. Mwanamke huyu ambaye hakufahamika jina,
umri, wala makazi yake alikuwa amevalia
nguo aina ya dera rangi ya njano. Mwili mehifadhiwa katika hospitali ya
muhimbili kwa utambuzi.
2.
Mtu mwingine VALERIAN S/O ERADIUS,
Miaka 13, Mwanafunzi wa kidato cha kwanza, shule ya sekondari Kigogo, Mkazi wa
Mburahati kwa Shebe amefariki dunia tarehe 10/05/2015 baada ya kuangukiwa na
ukuta kufuatia mvua kunyesha jijini Dar es Salaam. Mwili umehifadhiwa katika
hospitali ya taifa ya Muhimbili.
3.
Mnamo tarehe 08/05/2015 huko maeneo ya
Mbezi Beach Kilongamiwa Tarafa ya Kawe wilaya ya Kinondoni mtu mmoja aitwaye GERVAS S/O SHAYO, Miaka 28, shamba boy, mkazi wa Mbezi juu alikuwa amekufa maji. Mtoa
taarifa PROCHES S/O SEBASTIAN, Miaka 34, Mkazi wa Mbezi beach alisema taarifa
toka kwa mke wa marehemu zinasema siku ya tukio marehemu alisikika akiomba
msaada wa kuvushwa mtu huona baadaye hakurudi nyumbani hadi alipogundulika
akiwa amefariki dunia. Mwili wa marehemu umehifadhiwa katika hospitali ya
Mwananyamala kwa uchunguzi.
4.
Mtu mwingine mwanaume anayekadiriwa
kuwa naumsri kati ya miaka (35 – 38) ambaye jina, umri wala makazi yake
hayajajulikana mara moja ameopolewa katika tope leo tarehe 11/05/2015 maeneo ya
Magomeni Suna katika bonde la Mto Msimbazi akiwa tayari ameshafariki dunia.
Mwili wake umehifadhiwa katika hospitali ya taifa ya Muhimbili kwa uchunguzi na
utambuzi
Aidha,
uzoefu unaonyesha kuwa jinsi maji yanavyoendelea kupungua kutokana na kupungua
kwa mvua ndo madhara yanavyoendelea kuonekana. Nawataka wananchi waendelee
kutoa taarifa za mapema ili hatua zichukuliwe mara moja ikiwa ni pamoja na
kuiondoa miili ya watu watakaokuwa wamepoteza maisha kutokana na athari za mvua
zinazoendelea kunyesha katika jiji la Dar es Salaam.
Wananchi
wanaombwa kuzingatia taarifa zinazotolewa na mamlaka ya hali ya hewa kuhusu
hali ya hewa nchini ili wawe katika hali ya tahadhali ili kupunguza madhara
yanayoweza kutokea.
S. H. KOVA
KAMISHNA WA POLISI KANDA MAALUM
DAR ES SALAAM
No comments:
Post a Comment