Tuesday, May 12, 2015

KAMPUNI YA TIGO YATANGAZA MUENDELEZO WA USIMAMIZI

Kampuni ya Tigo Tanzania imetangaza kwamba Bw. Diego Gutierrez amerejea kama Meneja Mkuu wa Tigo Tanzania baada ya kumalizika kwa mkataba wa aliyekuwa akikaimu cheo cha Umeneja Mkuu Bi Cecile Tiano.

Kwa mujibu wa taarifa iliyotolewa kwa vyombo vya habari leo, Bi Tiano amekuwa kwenye kampuni ya Tigo kama Kiongozi wa muda tangu mwanzoni mwa mwaka huu. Amefurahia mafanikio makubwa aliyoyapata akiwa na kampuni ikiwa ni pamoja na kuzindua huduma ya Tigo Muziki na mtandao wa 4G, na kuifanya Kampuni ya Tigo kuwa ni Kampuni ya kwanza ya mawasiliano ya simu kutoa teknolojia nchini.


Pamoja na hitimisho la mafanikio ya miradi maalumu ambayo Bi Tiano aliianzisha ndani ya Kampuni akiwa kama Meneja Mkuu wa Muda, Bwana Gutierrez atatoa mwendelezo wa usimamizi kwa kukuza mipango mipya yenye mafanikio", Alieleza kwenye taarifa yake.

Maarifa ya Bw. Gutierrez kwenye biashara na katika soko yanatoa fursa ya kuweka biashara za mpito kwa pamoja. Kabla ya kuwa na kampuni kwenye kitengo ya fedha za kwenye simu za mkononi barani Amerika ya Kusini,alikuwa Meneja Mkuu wa Tigo Tanzania kwa muda wa miaka mitatu. Bw. Gutierrez ana uzoefu wa miaka 15 katika sekta ya mawasiliano ya simu, akiwa amefanya kazi katika masoko kadhaa Barani Amerika ya Kusini na Afrika. 

Nina furaha kwa mara nyingine kuendelea kufanya kazi na timu yenye shauku ya maendeleo ambayo kwa pamoja hushirikishana dira ya Tigo ya kuleta mabadiliko ya maisha ya kidijitali kwa Watanzania", Anasema Gutierrez katika taarifa yake.

No comments: