Monday, May 25, 2015

KUTOKA NEC--TAREHE RASMI YA KAMPENI NA SIKU YA UCHAGUZI HIZI HAPA


SIKU moja kupita baada ya chama cha Mapinduzi CCM kufungua Milango kwa Wanachama wake kuanza kuchukua Fomu za kuwania Uongozi mbali mbali ndani ya chama hicho kwenye Uchaguzi mkuu,nao pia Tume ya Taifa ya Uchaguzi nchini (NEC) imetangaza Rasmi tarehe ya Uchaguzi Mkuu, siku ya uteuzi wa Wagombe pamoja na siku ya kuanza kampeni za Uchaguzi  mkuu.Anaandika KAROLI VINSENT endelea nayo.


     
Kwa Mujibu wa Taarifa ya NEC kwa Vyombo vya Habari nchini iliyosainiwa na Mwenyekiti wa Tumr hiyo Jaji Mstaafu Damiani Lubuva ambapo inasema kuwa kwa Mujibu wa vifungu vya 35 B (1),(3)(a),37 (1) (a) na 46 (1),sura  ya 343, inaipa Mamlaka NEC kutangaza Ratiba hiyo.
        
  Pamoja na hayo amebainisha kuwa siku ya  Uteuzi wa Wagombea Urais,Ubunge na Udiwani utafanyika tarehe  21 Agosti mwaka huu,
Sanjari na hayo pia Kampeni za Uchaguzi nazo zitaanza tarehe 22Agosti mpaka tarehe 24 Octoba mwaka huu,
Ambapo Siku ya kupiga kura nchi nzima itafanyika tarehe 25 Oktoba mwaka huu.

       
  Kuibuka huko kwa NEC katika kutoa Ratiba ya Uchaguzi kunakuja Siku Moja kupita baada ya Mwenyekiti wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo Chadema Freeman Mbowe kumtaka Jaji Lubuva kuweka bayana utaratibu wa Uchaguzi ikiwemo siku ya Kampeni pamoja na Tarehe ya kupiga kura.

No comments: