Meneja mkuu wa kampuni ya Tigo, Diego Gutierez akifafanua jambo alipozungumza na wahariri wa kanda ya Ziwa jana kuhusiana na jinsi ambavyo Tigo imejipanga kuwekeza zaidi ya Sh2.6 bilioni katika kanda ya ziwa kwa mawaka huu.
Kampuni ya simu nza mkononi ya imetenga jumla
ya shilingi bilioni 2.6 kwa ajili ya kuwekeza katika ujenzi wa minara mipya na
kuboresha utoaji hudumakwa mikoa ya kanda ya ziwa kwa mwaka 2015.
Akiongea
na waandishi wa Habari wa mkoa wa Mwanza leo, Meneja mkuu wa kampuni ya Tigo
Diego Gutierrez amesema kwamba tigo itajenga minara mipya 63, minara hii
itajumlisha minara saba yenye uwezo wa kutoa huduma ya 4G LTE. Kanda ya Ziwa
inahusisha jumla ya mikoa nane, mikoa hii ni Mwanza, Shinyanga, Mara, Kigoma,
Kagera, Tabora, Geita and Simiyu.
Teknolojia
ya 4G LTE inamaanisha kasi na uwezo mkubwa wa kutembelea intaneti na kupakua
vitu mbalimbali na pia kupata huduma isiyosumbua ya Skype. Kasi hii pia
inawezesha wateja wa Tigo kupata huduma ya video pamoja na mikutano kwa kutumia
video (video conferencing), teknolojia hii ambayo tayari kampuni ya Tiggo
wanayo, ina kasi mara tano zaidi ya ile ya 3G.
“Kwa mwaka huu tunategemea kujenga minara mipya 63,
ili kuwawezesha wakaazi wa vijiji vyote vya mikoa hi inane ya kanda ya Ziwa
kupata huduma zetu, kwa wastani tutatumia jumla ya $ 100,000 kwa kila mnara,
hii inamaanisha kwamba tuttumia jumla ya dola 6.3 milioni kwa kanda ya Ziwa
pekee,” alisema Gutierrez.
“Kwa
hili tutakuwa tumewapatia wakaazi wa eneo la kanda ya Ziwa fursa mpya za
kijamii na kiuchumi kwa kuwapatia uwezo wa kuona yanayoendelea katika dunia
nyingine nje ya maeneo haya, kwa kutumia huduma ya intaneti tutakuwa pia
tumewapatia mageuzi ya kidijitali,” aliongeza Meneja Mkuu.
Kwa
mujibu wa Meneja Mkuu, Kanda ya Ziwa imekuwa ni eneo ambalo linafaidika zaidi
na ufadhili na shughuli mbalimbali za uwajibikaji kwa jamii (CSR) toka kampuni
ya Tigo, ambapo imekuwa ikisaidia jamii
katika maeneo ya elimu, afya, mazingira, ujasiriamali, kutengeneza ajira, sanaa
na michezo.
Katika
miaka miwili iliyopita, Tigo imewekeza wastani wa dola 2 milioni kwa wiki
katika mitandao yake hapa nchini. Uwekezaji huu ni pamoja na kupanua wigo wa
mitandao kwa kujenga minara mipya hata katika maeneo ya vijijini, kuboresha
teknolojia kwa kuleta teknolojia ya 3G ambayo imewezesha wananchi kujipatia huduma
ya data, kuwapatia mafunzo wafanyakazi na pia kutekeleza huduma za uwajibikaji
kwa jamii (CSR).
Gutierrez
pia alisema kwamba katika miezi 12 iliyopita Tigo imewezesha upatikanaji wa
huduma mbalimbali kwa wananchi, ikiwa ni pamoja kuwa kampuni ya kwanza nchini
kutoa huduma za kimataifa za kifedha zikiwa tayari zimeshawekwa katika viwango
vya nchi husika, uanzishwaji wa huduma ya Facebook kwa Kiswahili na pia
kuanzisha ushirikiano na watoa huduma wengine ili kuwawezesha wateja kutuma na
kupokea fedha kupitia mitandao mbalimbali iliyopo nchini.
Meneja
Mkuu aliongeza kwamba mafanikio yaliyopatikana ni pamoja na kuwapatia wateja
fursa ya ktoa na kuweka fedha katika akaunti mbalimbali za benki kwa kutumia
simu zao za mikononi, kuwapatia wateja gawio la faida kwa kila robo ya mwaka
katika akaunti zao za tigo pesa kutokana na salio lililopo, huduma ya muziki
kutoka Tigo ambayo inawapatia wateja uwezo wa kupata bila kikomo muziki kutoka
sehemu yeyote duniani kupitia Deezer na teknolojia ya 4G ambayo ilizinduliwa
mwezi uliopita.
|
No comments:
Post a Comment