Tuesday, May 5, 2015

picha--TIZAMA ALICHOKIFANYA MBOWE MUDA HUU HAPA UBUNGO

Mwenyekiti wa chama cha democrasia na maendeleo CHADEMA mh FREMAN MBOWE amewasili leo katika stend ya mabas ubungo kuzungumza na madereva ambao walikuwa wakiendeah mgomo wa kuwataka serikali iwasikilize shida zao.mh Mbowe ambaye aliwasili hapa majira ya saa nne kasoroo asubuhi alijikuta katika wakati mgumu baada ya wananchi kumshangilia kwa nguvu huku wengine wakifuta barabara ili gari yake ipite huku nyimbo zza ukawa zikiimbwa,jambo ambalo lilizua taharuki katika eneo hilo.Mh mbowe alipata nafasi ya kuzungumza na viongozi wa madereva hao.aidha viongozi kadhaa wa serikali waliokuwa katika eneo hilo walionekana kuzomewa na kutokuaminika na madereva hao.
Kuhusu mgomo huo Mkuu wa wilaya ya kinondoni mh PAUL MAKONDA amewaomba madereva hao kuendelea na kazi na ndani ya siku saba serikali itakua tayari imeshatoa tamko.
Madereva hao wamekubali kuanza safari kwa sharti la ndani ya siku saba wawe wamesikilizwa kero zao.MH MBOWE alipotaka kuzngumza na madereva hao microfone zote zilizimwa na kufichwa kusikojulikana jambo ambalo lilifanya ashindwe kusikika kwa madereva hao na kuamua kumtoa nje na kusukuma gari yake hadi maeneo ya shekilango na kurudi opfisini.Taarifa ni kuwa mgomo huo umekwishwa na magari hapa ubungo yameanza kutoka.
PICHA ZOTE ZA MBOWE UBUNGO ZIKO HAPA


No comments: