Waziri wa Kilimo Chakula na Ushirika, amnabe pia ni Mbunge Bunda mkoani Mara, Steven Masato Wasira leo ametangaza rasmi nia yake ya kuwania urais kwa tiketi ya Chama Cha Mapinduzi (CCM) katika uchaguzi mkuu utakaofanyikia baadae mwaka huu.
Katika hotuba yake ya takribani dakika 60 mh WASIRA ametumia muda mwingi kukemea vitendo vya rushwa hiuku akiwahmiza wananchi kumchagua kiongozi ambaye hatawaibia mali zao na badala yake wamchague mtu ambaye atawatumikia watanzania.
Amesema kuwa kiongozi anayekuja mbele za watu na kusema anaichukia ruswa wananchi wamwangalie usoni kama kweli anamaanisha anachoklisema au anasema kama fashion kwa sababu ameambiwa akisema anachukia rushwa atachaguliwa.
Amesema kuwa yeye ni kiongozi ambaye tangu tanzania imeanza kukumbwa na kashfa za wizi wa mali za umma hajawahi kutajwa wala kuhisiwa katika wizi huo hivyo anadhani yeye ni msafi na anafaa kuiongoza tanzania kwa miaka miktano ijayo
Wasira ametangaza siku moja baada ya Kada wa CCM na Waziri Mkuu Mstaafu na Mbunge wa Monduli, Edward Lowassa kulitika jiji la Arusha wakati akitangaza nia kama hiyo.Miongoni mwa makada wa CCM ambao wanatarajiwa kutangaza nia kama ya Lowassa na Wassira ni Naibu Waziri wa Fedha, Mwigulu Mchemba atakae tangaza nia hiyo baade leo, Charles Makongoro Nyerere, Lazaro Nyalandu, Bernard Membe, na makada wengine wengi wa chama hicho wametajwa kuwania nafasi hiyo.Wasira akitangaz nia hiyo hii leo katika Ukumbi wa BOT jijini Mwanza amesema yeye kauli mbiu yake ni Uadilifu.
No comments:
Post a Comment