Watu
waliopoteza maisha jijini Dar es Salaam kutokana na athari ya mafuriko kufuatia
mvua zinazoendelea kunyesha sasa imefikia kumi na tatu. Jeshi la Polisi Kanda
Maalum ya Dar es Salaam limethibitisha hilo ambapo mtu mmoja mwanaume
aliyetambulika kwa jina la EXAVERY S/O MICHAEL, Miaka 19, Mkazi wa Kingugi
Mbagala, alifariki dunia baada ya kusombwa na maji wakati akiwa katika harakati
za kuvuka mto Kizinga.
Tukio hili lilitokea tarehe 13/05/2015 majira ya saa
nane kamili mchana huko maeneo bonde la Mto Kizinga Kata ya Kiburugwa Wilaya ya
Temeke mkoa wa Dar es Salaam. Maiti yake iliopolewa na wasamaria wema na
imehifadhiwa katika Hospitali ya Temeke kwa uchunguzi na utambuzi.
Nawashukuru
wananchi kwa namna wanavyojitolea na kushiriki kushughulikia maafa
yanayoendelea kutokea ikiwa ni matokeo ya mafuriko yaliyosababisha na mvua
zinazonyesha mfululizo katika jiji la Dar es Salaam.
Nawaomba
wakazi wa maeneo yote ya jiji la Dar es Salaam waendelee kuchukua
tahadhali kwa kuwa madhara zaidi
yanaweza kutokea kutokana na kwamba mvua bado zinaendelea kunyesha. Aidha,
waendelee kutoa taarifa pindi wanapoona hali yoyote isiyo ya kawaida ili hatua
za haraka ziweke kuchukuliwa.
S. H. KOVA
KAMISHNA WA POLISI KANDA MAALUM
DAR ES SALAAM
No comments:
Post a Comment