Saturday, June 20, 2015

HAKIMU WA KESI YA MBOWE JUZI AKUTWA NA HAYA HAPA,MBOWE ATANGAZA JIMBO ATAKALOGOMBEA


Mwenyekiti wa Chama Taifa Freeman Mbowe akihutubia mkutano wa hadhara katika Uwanja wa Reli, Kata ya Njoro, Manispaa ya Moshi mjini jana.

 Akizungumzia hukumu iliyomtia hatiani na kuhukumiwa faini au kifungo, Mbowe ambaye pia ni Kiongozi wa Upinzani Bungeni alisema alikusudia kwenda jela kuwakilisha mamilioni ya Watanzania wanaosota huko “kwa kesi na hukumu za kipuuzi”.

“Kama kesi ya mtu mwenye dhamana ya uwakilishi wa wananchi kwa nafasi ya ubunge inaweza kuendeshwa kwa zaidi ya miaka minne na hukumu kutolewa katika mazingira tatanishi kama ilivyokuwa kwangu, Watanzania wa kawaida wanateseka kiasi gani?” 
alihoji Mbowe.

Alidai kuwa baada ya kumhukumu kifungo cha mwaka mmoja au faini ya Sh1,000,000, Hakimu Denis Mpelembwa amepandishwa cheo kuwa hakimu mkazi na kuhamishiwa mkoani Kagera, siku moja tu baada ya hukumu.

“Kilichokuwa kinatafutwa ni namna ya kumzuia Mbowe asigombee ubunge Hai kwa sababu CCM wanajua nguvu yangu. Wamekosea sana kwa sababu hukumu ile hainizuii kugombea. Nitaombea na nitashinda kwa kishindo,”

“Ninao wanasheria mahiri ambao baada ya kupitia hukumu yangu kwa harakaharaka, wamenihakikishia kwamba adhabu ile hainizuii kugombea na wanaendelea na taratibu nyingine za kisheria kuiomba Mahakama Kuu kuitangaza kuwa batili,” alisema.

No comments: