Wednesday, June 24, 2015

HALI BADO NI MBAYA KWA WAFANYAKAZI NCHINI TANZANIA-LHRC WAJA NA TAARIFA YA KUSHTUA,SOMA HII

Mwakilishi wa mgeni rasmi GODLISTERN NYANGE (katikati),mkurugenzi wa uwajibikajin na iuwezeshaji kutoka Kituo cha Sheria na haki za Binadamu EMELDA URIO (kulia) na wakili FLAVIAN CHARLES (Kushoto) kwa Pamoja wakiwa wanaonyesha Report ya Taarifa ya Haki za Binadamu na Biashara mara Baada ya kuizindua leo Jijini Dar es salaam
 Imeelezwa kuwa asilimia 99 ya wafanyakazi nchini Tanzania wanafanya kazi chini ya mikataba ambayo hawana ulewa nayo juu ya mgawanyo wa majukumu na kazi zao wawapo kazini
Hayo yameelezwa leo jijini Dar es salaam wakati wa uzinduzi wa taarifa ya haki za binadamu na biashara ya mwaka 2014 iliyozinduliwa leo na kituo cha sheria na haki za binadamu nchini Tanzania LHRC report ambayo imeeleza changamoto mbalimbali ambazo zinawakumba wafanyakazi nchini Tanzania.
Moja kati ya mambo ambayo yameanishwa katika report hiyo ambayo ilifanyiwa utafiti katika mikoa takribani  kumi na tano nchini Tanzania ni manyanyaso na changamoto mbalimbali ambazo zinawakuta wafanyakazi katika makampuni na sehemu mbalimbali ambapo zimeonekana kuwa kikwazo kikubwa kwa ustawi wa wafanyakazi na shughuli nzima za ajira nchini Tanzania.
Wadau mbalimbali wakikabidhiwa Nakala ya Taarifa hiyo mara baada ya kuzinduliwa leo
Akifafanua mambo ambayo yamegundukika katika tafiti ya report hiyo mmoja kati ya watafiti kutoka kituo cha sheria na haki za binadamu FLAVIAN CHARLES amesema kuwa maswala ya mikataba kwa wafanyakazi nchini yameendelea kuwa tatizo kubwa ambapo asilmia 99 ya wafanyakazi wamekuwa wakifanya kazi katika mikataba ambayo haielezi wazi majukumu yao halisi huku asilimia 25 ya wafanyakazi walisaini mikataba bila kuwa na makubaliano maalum na waajiri wao.
Aidha swala lingine ambalo limeonekana kuibuliwa na utafiti huo ni hali ya ubaguzi wa walemavu katika maeneo ya ajira ambapo zaidi ya asilimia 70 ya walemavu wanabaguliwa katika maswala ya ajira jambo ambalo limeelezwa kuwa baya sana ikizingatia kuwa walemavu ni watu wanaohitaji msaada wa karibu ili waweze kusonga mbele.


Katika hatua nyingine Report hiyo imeonyesha taifa kutafunwa na tatizo la ukwepaji wa kodi pamoja na biashara ya magendo ambapo imeeleza kuwa nchini Tanzania asilimia kubwa ya makampuni makubwa na wawekezaji wakubwa wenye uwezo wa kulipa kodi wamekuwa wakipata misamaha wa kodi huku watanzania wa kipato cha chini wakishushiwa mzigo huo kwa kuendelea kulipishwa kodi jambo ambalo limeelezwa kuwa linahitaji marekebisho makubwa ili taifa liweze kunufaika na wewekezaji waliopo nchini.
Picha ya pamoja na wadau mbalimbali walioshiriki katika uzinduzi wa Taarifa hiyo leo jijini Dar es salaam
Akizungumza wakati wa kuzindua Report hiyo GODLISTEN NYANGE ambaye ni Mkurugenzi wa Tafiti Tume ya sheria haki za binadamu na utawala bora nchini ambaye alimuwakilisha mwenyekiti wa tume hiyo amesema kuwa Report hiyo ya  haki za binadamu katika bishara imegusa eneo ambalo limesahaulika sana na mashirika mengi huku akisema kuwa itasaidia sana kufichua maswala mbalimbali wanayokutana nayo wafanyakazi katika maeneo kazi zao.

No comments: