Saturday, June 27, 2015

HUZUNI YATANDA DAR,MBOWE,DK SLAA WAUNGANA NA WANAHABARI KUAGA MWILI WA EDSON KAMUKARA


Pichani ni mkurugenzi wa magazeri ya halisi piblisher na mwandishi nguli wa habari za uchunguzi tanzania SAID KUBENEA akiuaga mwili wa mfanyakazi mwenzake EDSON KAMUKARA LEO Jijini Dar es salaam
Aliyekuwa mwandishi wa habari wa magazeti ya hali halisi publisher wazalishaji wa gazeti la mawio na mwanahalisi online Marehemu EDSON KAMUKARA leo mwili wake umeagwa Jijini Dar es saalaam na kusafirishwa kwenda kupumzishwa nyumbani kwao Bukoba baada ya kufariki ghafla Juzi Nyumbani kwake Mabibo Jijini Dar es salaam.
EDSON KAMUKARA alifariki Dunia Terehe 25 huu nyumbani kwake kwa kile kiinachotajwa kuwa ni ajali ya moto huku wengine wakisema ni ugonjwa wa malaria.
Habari za kifo chake zilianza kuenea kwa kasi majira ya saa kumi na mbili jioni ya siku hiyo ambapo Taarifa hizo zilikuwa zikieleza kuwa ndugu EDSONI KAMUKARA alifariki baada ya kulipukiwa na jiko la GESI lililokuwa ndani kwake huku Taarifa nyingine kinzani ambazo zinazidi kuenezwa zikidai kuwa ugonjwa wa malaria ndio uliosababisha kifo chake.
Katika shuguli hiyo ya kuaga mwili huo katika viwanja vya LEADERS leo asubuhi ilihudhuriwa na wadau mbalimbali wa maswala ya habari wakiwemo mwenyekiti wa wamiliki wa vyombo vya habari nchini Tanzania REGNALD MENGI,mwenyekiti wa chama cha democrasia na maendeleo CHADEMA Mh FREMAN MBOWE,pamoja na viongozi mbalimbali wa kiserikali na mashirika mbalimbali pamoja na wanahabari ambao ndugu EDSON  alikuwa akishirikiana nao kwa ukaribu.
Nimekuwekea picha mbalimbali za matukio katika shighuli hiyo huku tukizidi kufwatilia kwa ukaribu sababu za kifo hiki cha ghafla 

Wanahabari mbalimbali wakilia kwa uchungu wakati wa kuaga mwili EDSON KAMUKARA







































































No comments: