.

INAWEZEKANA HUJUI HILI KUHUSU MKE WA KAFULILA NA UBUNGE MWAKA HUU


Inawezekana ulikuwa hujui hili nalokupa kwa sasa--Mke wa Mbunge wa Kigoma Kusini kwa Tiketi ya Chama cha NCCR MAGEUZI Mh DAVID KAFULILA ambaye walifunga ndoa hivi majuzi JESCA KISHOA ni mwanachama wa chama cha Democrasia na maendeleo CHADEMA na Tayari ameanza harakati zake za kisiasa za kuhakikisha kuwa na yeye anamfuata mumewe Dodoma Mjengomi.

Katika mkutano wa hadhara wa baraza la wanawake la CHADEMA uliofanyika Jijini Dar es salaam hivi juzi mwanamama huyo alipanda jukwaani na kuwasalimia wanawake wa chama hicho huku akionekana kuwa mtu mwenye matumaini makubwa katika harakati zake hizo.

Baada ya kushukua jukwaani mwandishi wa Mtandao huu alipiga naye story kadhaa lakini miongoni mwa mambo ambayo Alitaka kufahamu ni kuhusu jimbo ambalo atagombea ubunge katika uchaguzi wa mwaka huu ambapo majibu yake ambayo hakuwa Tayari kuyatoa moja kwa moja alionyesha nia ya kutaka kumtoa mbunge wa  Iramba Magharibi MWIGUKU MCHEMBA ambaye kwa sasa amejikita katika kutafuta nafasi ya kugombea Urais wa Tanzania.
Kishoa anasema kuwa ana malengo ya kugombea nafasi ya ubunge katika jimbo la 
 Iramba Magharib kupitia chama cha democrasia na maendeleo CHADEMA kwa umoja wa UKAWA.
Nilitaka tu nikushirikishe hilo mdau,unaweza kutoa maoni yako
About HABARI24 TV

Post a Comment
Powered by Blogger.