Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa, Bernard Membe (kushoto), akibadilishana mawazo na Sheikh Mkuu wa Mkoa wa Dodoma, Mustafa Rajabu Shabani, wakati waumini wa Msikiti wa Gaddafi mkoani Dodoma, walipomwita jana kwa ajili ya kumshukuru kutokana na jitihada zake katika kuwezesha ujenzi wa msikiti huo uliojengwa kwa ufadhili wa aliyekuwa Kiongozi wa Libya, marehemu Muammar Gaddafi. Kulia ni Mwenyekiti wa Baraza Kuu la Waislam Tanzania (BAKWATA), Mkoani humo, Zidikheri Swedy Kheri.
|
No comments:
Post a Comment