Wafanyakazi wa mamlaka ya reli nchini Tanzania TRL wakiwa katika harakati za usafi mapema leo asubuhi ikiwa ni maadhimisho ya wiki ya mazingira nchini Tanzania |
Ikiwa dunia
inaadhimisha wiki ya mazingira duniani,wafanyakazi wa mamlaka ya Reli nchini Tanzania
TRL wameamua kutumia wiki hiyo katika kufanya usafi katika maeneo yote
yanayozunguka mamlaka hiyo ikiwa ni njia moja wapo ya kuweka mazingira safi na
kuadhimisha wiki hiyo ambayo huazimishwa kila mwaka kwa lengo la kuhamasisha
usafi katika mazingira mbalimbali.
Katika shughuli hizo ambazo
zilianza leo ndani ya TRL ampayo iliongozwa na viongozi mbalimbali kutoka
katika mamlaka hiyo akiwemo Mwenyekiti wa bodi,Mkurugenzi wa TRL na viongozi
mbalimbali kutoka shirika hilo linalotoa huduma za usafiri wa reli nchini Tanzania.
Mwenyekiti wa bodi ya TRL Bwana SEVERIN KAOMBWE akizungumza na wanahabari wakati wafanyakazi hao wakiendelea na usafi wa mazingira ya maeneo hayo |
Akizungiumza na
wanahabari wakati wa shughuli za usafi zikiendelea mwenyekiti wa bodi ya TRL
Bwana SEVERIN KAOMBWE amesema kuwa imekuwa ni mazoea kwa watanzania
kutokuyathamini mazingira yao kwa kuyafanyia usafi hivyo amewataka watanzania kujua
kuwa kitu muhimu katika mazingira yao ni kuyafanyia usafi.
Aidha amesema kuwa ni
lazima wafanyakazi hao wajiwekee utamaduni wa kuyafanyia usafi mazingira yao
kila siku ili yawe safi na sio kusubiri kipindi cha kuadhimisha siku ya
mazingira ndipo wayakumbuke mazingira hayo.
Naye mkuu wa idara ya
usafirishaji kutoka TRL Bwana LOLAND SIMTENGU amesema kuwa mamlaka hiyo ipo
katika uboreshaji wa mabehewa mbalimbali yanayotumika na abiria ili kuhakikisha
kuwa kuna vifaa vya kutosha vya kuweka taka taka ili kuondokana na uchafu
kuzagaa wkati wa safari huku akiwataka abiria watakaotumua vifaa hivyo kuwa
wazalendo kmuvitunza ili viweze kuwasaidia watanzania wenyewe..PICHA ZAIDI BONYEZA CHINI
No comments:
Post a Comment