Sunday, June 21, 2015

WASIRA AZINDUA BONGE LA BAND CHADEMA JIONI YA LEO,TIZAMA TUKIO NZIMA HAPA

Mwanachama wa chama cha Democrasia na maendeleo CHADEMA ambaye pia ni mwanaharakati wa maswala mbalimbali LILIAN WASIRA leo amezindua rasmi bendi yake ya music yenye lengo la kuwaamsha wanawake wa kitanzania kuamka na kuzipigania haki zao za msingi.
Lilian wasira ambaye kitaluma ni mwanasheria msomi ameszindua bendi hiyo leo katika viwanja vya TANGANYIKA PARKERS jijini Dar es salaam ambapo uzinduzi huo umefanyika rasmi na mwenyekiti wa chadema kanda ya pwani wakili MABERE MARANDO tukio ambalo limefanyika jioni ya leo jumapili.
Akizungumza na wanawake mbalimbali kutoka baraza la wanawake la chama cha demovrasia na maendeleo chadema BAWACHA p[amoja na mamia ya watanzania waliojitokeza kwa wingi LILIAN WASIRA amesema kuwa bendi hiyoi ameamua kuipa jina la WANAWAKE BAND ambapo amesema kuwa BAND hiyo sio mali ya chama cha democrasia na maendeleo chadema bali ni ya kwake binafsi lakini kwa kuwa yeye ni mwanachama wa chama hicho na mwanaharakati wa maswala ya haki za wananchi ameamua kuwa kazi ya kwanza ya BAND hiyo iwe ni kuwaamsha wanawake wa kitanzania kujiandikisha katika daftari la kupiga kura na baadaye kuwahamasisha kupiga kura na kuiondoa serikali ya CCM madarakani. PICHANI NI LILIAN WASIRA AKIWASILI KATIKA VIWANJA HIVYO


Amesema kuwa kampeni yta kwanza itakayofanywa na bendi hiyo itakwenda kwa jina la OPERATION AMSHA WANAWAKE TANZANIA operation ambayo amesema kuwa itaendeshwa katika mikoa zaidi ya 30 nchini tanzania kwa lengo la kukutana na wanawake na kuwahamasisha wanawake hao kufanya maamuzi sahihi kuelekea katika kipindi cha uchaguzi wa mwaka huu.
Naye mwenyekiti wa chama hicho kanda ya Pwani MABERE MARANDO amesema kuwa amefarijika sana kuona wanawake wa chama hicho kuwa wabunifu wa kiasi hicho cha kuanzisha band jambo ambalo amesema kuwa kwa sasa chadema itakuwa na uhakika wa kupata kura nyingi zaidi za wawake na hatimaye UKAWA kuichukua nchi hapo mwezi wa kumi..
Nimekuwekea picha mbalimbali za tukio nzima la uzinduzi wa BAND HIYO na jinsi wanawake walivyopagawishwa na music jioni hii
Wasanii mbalimbali kutoka chadema wakitoa burudani























No comments: