Tuesday, July 28, 2015

AZAM NA YANGA KESHO MTOTO HATUMWI DUKANI



Hatua ya Robo Fainali ya michuano ya Vilabu Bingwa Afrika Mashariki na Kati (Kagame Cup 2015) inatarajiwa kuendelea kesho Jumatano kwa michezo miwili kuchezwa katika uwanja wa Taifa jijini Dar es salaam, huku macho na masikio yakiwa kwenye mchezo kati ya Azam FC dhidi ya Yanga SC.

Mechi hiyo ya pili inatarajiwa kuanza saa 10:15 jioni inatarajiwa kuwa ya vuta nikuvute kufuatia timu hizo mbili zinatotokea jijini Dar es salaam kuwa na upinzani mkali kuanzia katika Ligi Kuu a Vodacom Tanzania na michuano mingine.


Kocha mkuu wa Azam FC, Stewart Hall amesema hana cha kuogopa katika mchezo huo dhidi ya Yanga, vijana wake amewandaa kupambana katika hatua hiyo ya robo fainali na ana imani wataibuka na ushindi.

Stewart ameongeza kuwa ana wigo mpana wa kikosi chake, katika hatua ya makundi wameweza kushinda michezo yao yote mitatu na kufunga mabao 8, huku ukuta wake ukiwa haujaruhusu bao hata moja kuingia wavuni kwake.

Kwa upande wa Yanga, kocha Hans Van der Pluijm amesema naaiheshimu klabu ya Azam, na katika mchezo wa kesho hana cha kupoteza, kikosi chake kimemalilika kila idara kuelekea katika hatua ya robo fainali.

Hans anajivunia kikosi chake ambacho kimeonyesha mabadiliko makubwa kutoka mchezo wake wa awali iliyoupoteza, na kushinda michezo mitatu mfululizo iliyofuatia katika hatua ya makundi.

Mchezo wa kwanza wa robo fainali utazikutanisha timu za KCCA ya Uganda dhidi ya Al Shandy ya Sudan, mechi itakayoanza saa 7:45 mchana uwnaja wa Taifa jijini Dar es aalaam.

Wakati huo huo Mkurugenzi Mtendaji wa Benki ya NMB nchini Tanzania Ineke Bussemaker anatarajiwa kuwa mgeni rasmi katika mchezo wa robo fainali kesho kati ya Azam FC dhidi ya Yanga SC.


RAIS WA FFB KUWASILI LEO
Rais wa Shirikisho la Mpira wa Miguu nchini Burundu (FFB), Reverien Ndikuriyo anatarajiwa kuwasili leo saa 5 usiku jijini Dar es salaam kwa shirika la Ndege la Rwanda Air.

Ndikuriyo anatarjaiwa kuwa na mazungumzo na Rais wa TFF, Jamali Malinzi kisha atashuhudia michuano ya kombe la Kagame inayoendelea kutimua vumbi jijini Dar es salaam ikiwa katika hatua ya robo fainali kwa sasa.

Aidha Vicent Nzamwita Rais wa Shirikisho la Mpira wa Miguu nchini Rwanda (FERWAFA) anatarajiwa kuwasili nchini alhamis akiambatana na kocha wa timu ya Taifa ya Rwanda (Amavubi) John McKinstry.

Rais wa FERWAFA anatarajiwa kuwa na mazungumzo na Rais wa TFF, Jamal Malinzi na baadae kuhudhuria michuano ya Kombe la Kagame inayoendelea nchini Tanzania.



IMETOLEWA NA SHIRIKISHO LA MPIRA WA MIGUU TANZANIA (TFF)

No comments: