Wednesday, July 29, 2015

KUTOKA OFISI YA MAKAMU WA RAIS DKT. BILAL LEO

MAKAMU WA RAIS DKT. BILAL AKUTANA NA UONGOZI WA SUMATRA, TRA, TABOA, RC-DSM NA WAZIRI WA FEDHA IKULU KWA MAZUNGUMZO.
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal, akizungumza na Baadhi ya Viongozi wa Chama cha Wamiliki wa Mabasi Tanzania (TABOA) TRA, SUMATRA, Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam na Waziri wa Fedha, wakati  walipofika Ofisini kwake Ikulu jijini Dar es Salaam, leo Julai 29, 2015. Picha na OMR


Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal, akiwa katika picha ya pamoja na baadhi ya viongozi wa SUMATRA, TRA, na Wamiliki wa Mabasi Tanzania TABOA, Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam, na Waziri wa Fedha, baada ya kumalizika kwa mazungumzo yao yaliyofanyika Ofisini kwa Makamu Ikulu jijini Dar es Salaam,leo Julai, 29, 2015. Picha na OMR
 MAKAMU WA RAIS DKT. BILAL, AKUTANA NA WAFANYABIASHARA WA ECG NA AL KAN KUTOKA MISRI, IKULU DAR
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal, akizungumza na Wafanyabiashara wa ECG na Al Kan kutoka nchini Misri, wakati walipofika Ofisini kwake Ikulu jijini Dar es Salaam, leo Julai 29, 2015 kwa mazungumzo. Picha na OMR

Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal, akiwa katika picha ya pamoja na Wafanyabiashara wa ECG AL Kan kutoka nchini Misri, baada ya kumalizika kwa mazungumzo yao yaliyofanyika Ofisini kwa Makamu Ikulu jijini Dar es Salaam,leo Julai, 29, 2015. Picha na OMR


No comments: