Wednesday, July 29, 2015

Tigo yazindua Duka Jipya Ifakara

ifakara picha no 1
Katibu Tawala wilaya ya Kilombero ndugu Yahya Naniya akikata utepe ikiwa ni ishara rasmi ya  uzinduzi wa duka la Tigo lililopo Ifakara mjini, kutoka kushoto ni Meneja wa operesheni kwa wateja Tigo kanda ya Pwani, Isack Shoo, Inspekta Dotto Ngimbwa kutoka ofisi ya OCD Kilombero na mwisho kulia  Mkurugenzi wa Tigo kanda ya mashariki Goodluck Charles.
ifakara picha no 7
Mkurugenzi wa Tigo kanda ya mashariki, Goodluck Charles akizungumza machache kwenye hafla hiyo kabla ya kumkaribisha mgeni rasmi.
ifakara picha no 8
Katibu Tawala wilaya ya Kilombero ndugu Yahya Naniya, akizungumza na wageni waalikwa kwenye hafla hiyo fupi ya uzinduzi wa duka la Tigo lililopo Ifakara mjini.
ifakara picha no 2
Wafanyakazi wa duka la Tigo lililopo Ifakara mjini wakipozi kwenye picha ya pamoja na mgeni rasmi aliyevaa tai nyekundu ndugu Yahya Naniya ambae ni Katibu Tawala wa wilaya ya Kilombero, muda mfupi baada ya hafla fupi ya uzinduzi wa duka hilo.
ifakara picha no 4
Meneja wa operesheni kwa wateja Tigo kanda ya Pwani, Isack Shoo akitoa maelekezo jinsi watakavyo hudumia wateja kwa mgeni rasmi Katibu tawala wa wilaya ya Kilombero ndugu Yahya  Naniya baada ya uzinduzi wa duka hilo lililopo Ifakara mjini.
ifakara picha no 5
Muonekano wa duka jipya kwa wateja wa Tigo lililopo Ifakara mjini.
ifakara picha no 6
Mgeni rasmi katika hafla ya uzinduzi wa duka la Tigo Ifakara mjini ndugu Yahya  Naniya ambae ni Katibu tawala wa wilaya ya Kilombero (wapili kutoka kulia) akiwa katika meza kuu na  Goodluck Charles Mkurugenzi wa Tigo kanda ya mashariki(wa pili kushoto)  Inspekta Dotto Ngimbwa kutoka ofisi ya OCD Kilombero(kushoto) na Meneja wa operesheni kwa wateja Tigo kanda ya Pwani, Isack Shoo (kulia).
 

No comments: