Wednesday, August 12, 2015

KUTOKA DRFA MCHANA HUU


MAAMUZI YA KAMATI YA UCHAGUZI YA DRFA KUHUSU RUFANI ZA WAGOMBEA WA NAFASI MBALIMBALI  ZA UONGOZI WA CHAMA CHA SOKA WILAYA YA TEMEKE (TEFA) KUPINGA MAAMUZI YA KAMATI YA  UCHAGUZI YA TEFA.      ZILIZOSIKILIZWA TAREHE 10/08/2015 KATIKA  HOTELI YA PR TEMEKE.







WAJUMBE WALIOHUDHURIA NI:
1.      RASHID SAADALLAH-MWENYEKITI
2.      FAHAD F.A. KAYUGA-KATIBU
3.      JUMA PINTO-MJUMBE
4.      HAJI BECHINA-MJUMBE
 
 
   1. RASHID SALIM-NAFASI YA MWENYEKITI WA TEFA
-Kashindwa kuleta vielelezo kuthibitisha uzoefu wake katika masuala ya mpira kama Ibara ya 31(1)(j) inavyosema,  alidai kuwa amekuwa kiongozi wa Tandika FC kwa muda wa miaka saba lakini hukuweza kuthibitisha maelezo yake kwa vielelezo. Kwa hivyo kamati inakubaliana na maamuzi ya kumuengua ya kamati ya uchaguzi TEFA.
 
 
 
 2. PETER STEPHEN MUHUNZI-NAFASI YA MWENYEKITI WA TEFA
-Kathibitisha kigezo cha elimu kwa maana ya kumaliza kidato cha nne ingawa kuna pingamizi la matumizi mabaya ya fedha na ubadhirifu, haya kamati yangu haina mamlaka ya kuyatolea maamuzi hivyo yanapelekwa kwenye kamati ya maadili ya DRFA.
 
   3. AZIZ MOHAMED KHALFAN-NAFASI YA MWENYEKITI WA TEFA
 -kamati imegundua kwamba alienda kwenye mchakato wa uchaguzi akiwa hana sifa kwa sababu alifungiwa na kamati ya nidhamu na usuluhishi ya kutokushiriki au kujihusisha na mpira kwa muda wa miezi kumi na mbili (12) na TEFA hata hivyo hakukata rufaa juu ya kifungo hicho na badala yake alikwenda kupeleka malalamiko yake TFF. Kiutaratibu baada ya kufungiwa na kamati tajwa alipaswa akate rufaa katika kamati ya rufaa ya TEFA, na kama asingeridhika na maamuzi ya kamati ya rufaa ya TEFA ndiyo angeweza kukata rufaa katika kamati ya uchaguzi ya DRFA. Kwa maana hiyo kamati inamuengua kwa sababu rufaa yake imeshindwa kuzingatia kanuni na taratibu za kukata rufaa.
       
4. SIZZA CHENJA-NAFASI YA MWENYEKITI WA TEFA
-kamati imempitisha aendelee na mchakato wa uchaguzi baada ya kuthibitisha kuwa ana uzoefu wa kutosha katika uongozi wa mpira wa miguu kama katiba ya TEFA Ibara ya (31)(1)(j) inavyotaka. Kwani mnamo mwaka 2009 alikua kiongozi katika klabu ya soka ya Tp Vita vilevile ameweza kushiriki ugombea katika nafasi ya ujumbe wa kamati ya utendaji wa DRFA katika vipindi tofauti ikiwemo mwaka 2012 ambapo alishindwa kupata nafasi hiyo.
 
5. OMARY. A. KAPILIMA-NAFASI YA MAKAMU YA KWANZA WA  MWENYEKITI
-kaweza kuthibitisha uzoefu wa uongozi wa mpira lakini kashindwa kuleta cheti cha kidato cha nne kinachotambulika na Baraza la Mitihani la Taifa yaani (NECTA). Hivyo maamuzi ni kuwa kashindwa kukidhi kigezo cha elimu kama inavyotakiwa na Ibara ya 31(1)(b) ya katiba ya TEFA.
 
 
 
 
6. SALEHE MOHAMED SALEHE-NAFASI YA MAKAMU WA KWANZA WA MWENYEKITI
Kamati inamuengua katika mchakato wa uchaguzi kwa kushindwa kuthibitisha kiwango chake cha elimu kwa kushindwa kuleta cheti cha kidato cha nne(Academic Certificate) kama inavyotakiwa na Ibara ya 31(1)(b) ya katiba ya TEFA. Pia  kulikuwa na madai ya ubadhirifu wa fedha na kuuza timu ya Tesema FC akiwa kama makamu wa kwanza wa mwenyekiti wa TEFA, haya kamati inayapeleka katika kamati ya maadili ya DRFA kwa ufafanuzi na maamuzi.
 
7. SHUFAA JUMANNE- NAFASI YA MAKAMU WA KWANZA WA MWENYEKITI
-Kamati inampitisha aendelee na mchakato wa uchaguzi baada ya kuridhika na uthibitisho wa uzoefu wa zaidi ya miaka mitatu katika uongozi wa soka. Ameweza kuithibitishia  kamati kwa vielelezo kuwa amekuwa kiongozi wa Tale FC kwa zaidi ya miaka mitatu. Vilevile ameleta vielelezo kuthibitisha kuwa Tale FC ni mwanachama hai wa TEFA kinyume na madai ya mpingaji.
 
8. DAUDI FRANCIS MUMBULI-NAFASI YA MAKAMU WA KWANZA WA MWENYEKITI
-Kamati inaitupilia mbali rufani hii baada muweka pingamizi kushindwa kutokea mbele ya kamati kuthibitisha madai yake. Hivyo maamuzi ya kamati ya uchaguzi y a TEFA yanabaki kama yalivyo. .
 
9. BAKILI M. MAKELE-NAFASI YA MAKAMU WA PILI WA MWENYEKITI
-Kamati imemuengua katika mchakato wa uchaguzi kwa kigezo cha elimu, kama inavyotakiwa na Ibara ya 31(1)(b) ya katiba ya TEFA . Mgombea amekiri kwamba elimu yake ni ya darasa la saba.
 
 
 
10. AMACK NABOLA- NAFASI YA UJUMBE SOKA LA WANAWAKE NA VIJANA
-Kamati inamuengua katika mchakato kwa kukosa sifa ya elimu ya kidato cha nne kama ibara ya 31(1)(b) ya katiba ya TEFA inavyotaka. Amack Nabola anagombea nafasi ya ujumbe wa soka la wanawake na vijana hivyo halindwi na ibara ndogo katika ibara ya 31 ambayo inatoa sifa za mgombea nafasi ya ujumbe wa kamati ya utendaji  kwa kumtaka mjumbe awe na elimu isiyo chini ya darasa la saba.  Ibara hii ipo kwa ajili ya wagombea wanaogombea nafasi za ujumbe wa kamati ya utendaji na si wajumbe wa makundi mbali mbali kama vile kundi la wanawake na vijana.
11. FIKIRI MAGOSO-NAFASI NI MJUMBE WA KAMATI YA UTENDAJI  
-Kamati inampitisha kugombea nafasi hii kwa sababu anakidhi vigezo kwa kuwa na cheti cha darasa la saba kama katiba ya TEFA anavyomtaka mgombea wa nafasi ya ujumbe wa kamati ya utendaji kuwa na elimu isiyo chini ya darasa la saba.
 
12. MUHIBU KANU MSHANGAMA- MAKAMU MWENYEKITI NA MJUMBE KAMATI YA UTENDAJI.
Kamati inamuengua kwa sababu  ni kinyume cha kanuni za uchaguzi za TFF za mwaka 2013 (TFF ELECTORAL CODE) Ibara 10(9) ambayo inakataza mgombea kugombea nafasi zaidi ya moja. Muhibu Kanu Mshangama anagombea nafasi ya makamu mwenyeki wa pili na mjumbe wa kamati ya utendaji kupitia kanda tandika.
 
MWENYEKITI
RASHID SADALA (ADVOCATE)

No comments: