Wednesday, August 12, 2015

Ne-Yo kutumbuiza Coke Studio Africa nchini Kenya na nyota wa Afrika

Kufuatia tetesi mbalimbali kuhusu ujio wa mkali wa miondoko ya R&B na Pop NE-YO katika onyesho la Coke Studio Afrika msimu wa tatu, sasa imethibitishwa kuwa msanii huyo atakuja rasmi.

NE-YO ambaye atakuwa ndiye mgeni pekee kutoka nje ya Afrika, ataambatana na nyota wengine wa Afrika ambao ni Wangechi (Kenya), Alikiba  (Tanzania), Maurice Kirya (Uganda), Dama Do Bling (Mozambique) na Ice Prince (Nigeria) ambapo wataungana kufanya nyimbo moja.

Kuelekea ujio wake nchini Kenya, NE-YO  ametoa taarifa rasmi ambayo inasema, “ Ni heshima kubwa sana kwangu kurejea Afrika na kushirikiana na wasanii kutoka bara hili, kupitia Coke Studio Afrika, hii ni fursa nzuri inayojenga uhusiano mzuri miongoni mwa watu wa rangi , makabila na dini zote kujumuika kwa pamoja katika onyesho hili la kukumbukwa.. Nimefurahi sana kupata wasaa huu wa kujumuika na wasanii na wanamuziki hawa wenye vipaji vikubwa kabisa.

Mwezi uliopita alitumbuiza katika tuzo za MTV Music ambazo zilifanyika nchini Afrika Kusini. Akiwa nchini Kenya NE-YO  ataungana na nyota watano kutoka nchini za Kenya, Nigeria, Tanzani, Uganda na Msumbiji kufanya wimbo wa pamoja kwa ajili ya msimu mpya. Hata hivyo wasanii hao wote kutoka katika nchi hizo wameshafanya wimbo wa pamoja.

Ndani ya miaka 10, NE-YO ametoa albamu sita. Albamu yake ya kwanza kabisa ni My Own Words was a bona fide R&B game changer bearing classics: “Stay”, “So Sick”, “When You’re Mad” and “Sexy Love”. Albamu yake ya hivi karibuni ya Non–Fiction, iliachiwa mwezi Januari mwaka huu. Albamu hiyo ilishika nafasi ya tano nchini Marekani miongoni mwa albamu 200 bora, na kumfanya NE-YO kuwa mwanamuziki wa kiume wa pili kuwa na albamu 6 mfululizo zilizoingia kumi bora.

NE-YO amefanikiwa kujikusanyia tuzo mbalimbali ulimwenguni na kuwa miongoni mwa watunzi mahiri wa nyimbo zinazotikisha ulimwenguni, ikiwemo ile aliyoshirikiana na Rihana ya “Unfaithful” and Beyonce’s “Irreplaceable”. Hivi karibuni NE=YO ametangazwa kujiunga na moja vipindi maarufu vya ‘series’ za runinga cha ‘Empire’ kama mtunzi wa mziki, msimu wa pili wa ‘Empire’ unatarajiwa kuanza mwezi Septemba.

 katika Coke Studio Afrika msimu wa 2  mwaka jana, mwanamuziki Wyclef Jean alitumbuiza wimbo wake uliokuwa ukitikisa wa “Divine Sorrow”, akipewa ushirikiano wa karibu na wasanii wengine wakiwemo Rabbit, Chidinma na Shaa.

Mpaka sasa katika msimu huu wa tatu, imeshuhudiwa wanamuziki kama Chameleone, Olamide, Jua Cali, Elani, Vanessa Mdee, 2 Face Idibia, Fid Q, Juliana Kanyamozi na Neyma na wengine wakiwa tayari wamesharekodi wimbo wao wa pamoja

Muwania tuzo ya Grammy, ambaye ni mwanamuziki na muandaaji pia Zwai Bala kutoka kundi la TKZee maarufu kwa mziki wa Kwaito nchini Afrika Kusini, amekuwa ndio muongozaji huku Brett Lotriet, muongozaji na muandaaji maarufu wa kimataifa wa runinga atakuwa ndiye muandaaji wa mlolongo wa matukio yanayorekodiwa.

Kwa kuongezea, wanamuziki kwa kushirikiana na bendi yenye watu wenye vipaji vya aina yake watatoa wimbo mpya kila wiki ambao utaandaliwa kwa pamoja na waandaaji wa ndani na kimataifa. Baadhi ya waandaaji hao ni Odongo, Eric Musyoka na Kevin Provoke kutoka Kenya, Cobhams Asuquo, Masterkraft na  Chopstix kutoka Nigeria, Owour Arunga kutoka Marekani, Nahreel kutoka Tanzania na Silvastone kutoka Uingereza.


Lengo kuu la Coke Studio Afrika ni kuwakutanisha kwa pamoja wasanii  mbalimbali wa Afrika na kuimba nyimbo ambazo zina vionjo tofauti hivyo kuongeza msisimuko. Lakini vilevile kutoa fursa kwa wasanii wachanga  kushirikiana na wakubwa ili kuwapa changamoto ya kuongeza ujuzi katika kazi zao na kuzidi kukuza vipaji vyao

No comments: