Friday, August 7, 2015

Taarifa mpya Kuhusu dk slaa kurejea ofisini


Salaam.

Vyombo vya habari kadhaa vimeendelea kuripoti kuhusu Katibu Mkuu wa Chama, Dk. Slaa Kwa namna mbalimbali, Kwa leo vipo vilivyohabarisha kuwa atarejea Ofisini leo.

Naomba kusaidia katika hilo ili kupunguza usumbufu usiokuwa wa lazima kwa wanahabari (ambao wanataka kujua itakuwa saa ngapi), wanachama, wapenzi, mashabiki na wafuasi wa CHADEMA kwamba;

Kurejea kwa Dk. Slaa ofisini baada ya kumaliza likizo ya kutafakari aliyokubaliana na chama, hakutakuwa kwa siri.
Haitafanywa siri kwa sababu; kwanza hata mapumziko yake hayo hajafanywa siri. Ufafanuzi ulitolewa Kwa uzito mkubwa na Mwenyekiti wa Chama Taifa, Freeman Mbowe.

Pili hakuwezi kuwa siri kwa sababu vyovyote vile kwa viwango vya habari, hiyo itakuwa ni habari kubwa kwa vyombo vya habari na umma wa Watanzania.
Tatu; haitakuwa siri Kwa sababu wanachama watapenda kushiriki jambo hilo.

Hivyo basi mara Dk. Slaa atakapomaliza mapumziko ya kutafakari na akarejea ofisini, Kwa uzito ule ule uliotumika kusema kuwa yuko likizo aliyokubaliana na chama, tutawataarifu Watanzania wote, vikiwemo Vyombo vya Habari ili visiendelee kuandika tetesi ambazo zinawasababishia usumbufu wananchi na waandishi wengine.
Makene

No comments: