Monday, August 31, 2015

TASWA FC, TASWA QUEENS WAMALIZA ZIARA YAO YA MKOA WA ARUSHA NA TANGA BILA KUFUNGWA, TASWA QUEENS WAIBUKA MABINGWA WA BONANZA LA TASWA ARUSHA

Kikosi cha Taswa Fc

Mchezaji wa Taswa Fc, Martine Peter, akimtoka mchezaji wa timu ya IMS Maji ya Chai, wakati wa mchezo wa Bonanza la 10 la Taswa Arusha lililofanyika mwishoni mwa wiki kwenye Uwanja wa Sheikh Amri Abeid, jijini Arusha. Katika mchezo huo timu hizo zilitoka sare ya 1-1.

Hussein Omari na Imman Makongoro wa Taswa Fc na Taswa Queens, wakifurahia baada ya kukamata Kuku katika mchezo wa kukimbiza kuku kwenye Bonanza la 10 la Taswa Arusha mwishoni mwa wiki jijini Arusha.

Mchezaji wa Taswa Queens, Oliver Arbogasti, akimiliki mpira wakati wa mchezo wao na timu ya Chuo cha Waandishi wa Habari cha Arusha AJTC. Katika mchezo huo Taswa Queens, ilishinda mabao 37 - 3.

Kikosi cha timu ya Taswa Queens. 

Nahodha wa timu ya Taswa Queens, Zuhura Abdulnoor, akipokea zawadi ya Sh. 150,000, kutoka kwa Mkuu wa Mkoa wa Arusha, Daud Ntibenda, baada ya kutangazwa washindi wa Bonanza la 10 la Taswa Arusha lililofanyika mwishoni mwa wiki kwenye Uwanja wa Sheikh Amri Abeid jijini Arusha. 

Nahodha wa timu ya Taswa Queens, Zuhura Abdulnoor, akipokea Kikombe cha ushindi kutoka kwa Mkuu wa Mkoa wa Arusha, Daud Ntibenda, baada ya kutangazwa washindi wa Bonanza la 10 la Taswa Arusha lililofanyika mwishoni mwa wiki kwenye Uwanja wa Sheikh Amri Abeid jijini Arusha. Picha na


Mwenyekiti wa Taswa Majuto Omary, akipokea zawadi ya fedha kutoka kwa Mkuu wa Mkoa wa Arusha, Daud Ntibenda, baada ya timu yake kutangazwa kuwa timu yenye nidhamu katika mashindao ya Bonanza la 10 la Taswa Arusha, lililofanyika mwishoni mwa wiki kwenye Uwanja wa Sheikh Amri Abeid jijini Arusha. 

Kikosi cha timu ya Taswa queens.

Mchezaji wa Taswa Fc, Zahro Mlanzi, akimtoka mchezaji wa timu ya IMS Maji ya Chai, wakati wa mchezo wa Bonanza la 10 la Taswa Arusha lililofanyika mwishoni mwa wiki kwenye Uwanja wa Sheikh Amri Abeid, jijini Arusha. Katika mchezo huo timu hizo zilitoka sare ya 1-1

Baadhi ya waandishi wa habari za Michezo kutoka Vyombo mbalimbali vya habari, wanaounda timu ya Waandishi wa habari za Michezo Tanzania, Taswa Fc na Taswa Queens, wakimsikiliza Afisa wa Hifadhi ya Michael  Ngatolu, wakati walipotembelea kwenye hiyo, walipokuwa katika ziara ya kuhitimisha Bonanza la 10 la Taswa Arusha lililofanyika mwishoni mwa wiki kwenye Uwanja wa Sheikh Amri Abeid jijini Arusha. 
TIMU ya Taswa Fc na ile ya Taswa Queens, zinazoundwa na wachezaji wa Habari za Michezo kutoka vyombo mbalimbali vya habari Tanzania, jana ilihitimisha ziara yake ya siku mbili katika mikoa ya Arusha na Tanga.

Aidha timu hiyo ilifanikiwa kumaliza ziara hiyo bila kufungwa huku Taswa Queens, wakiibuka kidedea kwa kutwaa Ubingwa wa mashindano ya Bonanza la Taswa Arusha yanayofanyika kila mwaka, baada ya kuwagalagaza bila huruma timu ya Chuo cha Waandishi wa Habari cha Arusha AJTC kwa jumla ya mabao 37-3.

Wakati Taswa Queens ikitwaa Kombe hilo, Taswa Fc, wao walimaliza bonanza hilo bila kufungwa huku wakitoka sare katika michezo yake yote mitatu.

Katika mchezo wa kwanza Taswa Fc ambayo ilidhaminiwa na Mamlaka ya Hifadhi ya Ngorongoro, ilitoka sare ya bila kufungana na timu ya ORS ya Manyara, kabla ya kutoka sare ya bila kufungana tena na timu ya IMS Maji ya Chai, na baadaye kutoka sare ya bao 1-1 na timu ya Kampuni ya Habari Maalum ya Arusha.

Baada ya Bonanza hilo Taswa Fc, walielekea Tanga Segela na kucheza mchezo wake wa mwisho na timu ya Kombaini ya Segera na Michungwani na kuibuka washindi kwa mabao 2-0 katika mchezo uliokuwa mkali na wa kuvutia kutokana na timu zote kucheza kwa speed na kukamiana huku wachezaji wakionyesha uwezo wa hali ya juu.

No comments: