Thursday, August 6, 2015

Wakati CUF kuna giza nene,Hii imetokea buguruni jioni hii,usikose mdau


Muda mfupi uliopita nimepita katika viwanja vya buguruni sheli ambapo leo chama cha ALLIANCE FOR DEMOCRATIC CHANGE (ADC) wamefanya mkutano mkubwa  wa hadhara wenye lengo la kuwatambulisha wagombea wao wa nafasi za Urais wa Tanzania na ule wa zanzibar kwa wananchi ambapo mkutano huo umehudhuriwa na mamia ya wanachama na wakazi wa maeneo ya karibu na viwanja hivyo.

Pichani katikati ni mgombea wa nafasi ya Urais wa jamhuri ya muungano wa Tanzania CHIEF LIEMBA akiwa amemshika mkono mgombea wa nafasi ya Urais wa serikali ya mapinduzi ya zanzibar HAMAD RASHID kulia kwake,huku kushoto akiwa ni mgombea mwenza wa urais wa Jamhuri ya muungano wa Tanzania SAID MIRAJ wakati wakijitambulisha kwa mara ya kwanza kwa wananchi tangu wateuliwe na mkutano mkuu kupeperusha bendera ya chama hicho katika uchaguzi mkuu wa mwaka huu.
Hapa nimekupa uhondo wa picha zaidi ya 20 za mkutano huo uliomalizika muda mfupi uliopita hapa Buguruni Jijini Dar es salaam















No comments: