Rais wa chama cha walimu nchini TANZANIA Bwana GRATIAN MUKOBA akizungumza na wanahabari mapema leo Jijini Dar es salaam |
Chama cha walimu nchini
Tanzania CWT kimeitaka serikali kukamilisha madai ya walimu hadi ifikapo September
mwaka huu.
Akizungumza na
wanahabari mapema leo Rais wa chama hicho Bwana GRATIAN MUKOBA amesema kuwa
serikali imekuwa ikupuuza madai ya walimu hao kwa muda mrefu sasa ambapo
amesema kuwa mnamo agost tatu mwaka huu
serikali kupitia wizara ya elimu ilikutana na walimu ili kujadili mambo
mbalimbali ikiwemo muundo mpya wa kazi na malipo ya walimu lakini bado serikali
haikutoa majibu ya moja kwa moja kuwa itatatua changamoto hizo lini .
Aidha Bwana MUKOBA
amesema kuwa sheria ya malipo ya walimu katika kada mbalimbali inaelekeza kuwa
mishahara iendane na posho ambapo hadi kufikia leo hakuna posho yoyote
iliyotolewa kwa mwalimu yeyote hali inayopelekea deni la walimu kufikia billion
tano hadi sasa .
Sambamba na hilo MUKOBA
amebainisha kuwa kuna baadhi ya wastaafu ambao hawajalipwa malipo yao tangu
mwezi wa nane mwaka jana hali inayowafanya wastaafu hao kubaki omba omba katika
maeneo mbalimbali nchini.
Hata hivyo Bwana Mukoba
ameongeza kuwa ni lazima serikali itenge hela zinazotosha kulipa madeni yote ya
walimu ili kuhakikisha kuwa walimu wanarudisha ari na muamko wa utekelezaji wa
majukumu yao ya kujenga taifa na kuboresha mazingira yao ya utoaji wa elimu.
Katika hatua nyingine
MUKOBA amesema kuwa mnamo mwezi ujao kutakuwa na mkutano mkuu wa walimu hao
ambao pamoja na mambo mengine mada kuu watakuwa wakiangalia serikali
imetekelezaje madai hayo waliyoyatoa kabla ya kujadili kwa kina mambo ya kufanya
kuelekea uchaguzi mkuu wa mwaka huu.
No comments:
Post a Comment