Gwajima anaonyesha meseji aliyotumiwa na Dr. Slaa kuhusu
kustaafu kwake siasa
Gwajima: Kama Dr. Slaa anakaja aje atoke hapa akane aone mambo ya mshenga
yalivyo, watu wanashangaa Slaa anaweza kufanya haya! Si yeye ni mama. Slaa
alikuwa adili, sasa uzoefu wa ndoa hana, bora sisi wachungaji tunaoa.
Nilimpa maneno ya matumaini, nitamtafuta mkewe niongee nae, nilimtafuta mkewe
rose garden. Nilianza mimi kumbembeleza amruhusu baba aendelee na hayo maelezo
nimeyarokodi na mimi ni mtu wa kurekodi. Alisema ameshawaambia watu yeye
atakuwa first lady, siku iliyofata tarehe 28, nilimuita yule mama Kibo complex.
Tukakaa ndani ya gari yake, nilikuwa mimi na mtu mwingine, niliendelea kurekodi
tena. Ilikuwa ni siku Lowassa anapokea kadi bahari beach, nawaonyesha hio sio kwa
mumuone Slaa mbaya. Saa nane mchana akasema nimekubali Slaa arudi aingie kazini
kwa sharti mkutano wa kumpokea Lowassa ufutwe. Nikamwambia hilo halitatokea
milele.
Watu wengi sana wametumwa kuongea na yule mama, akiwemo mzee Ndesamburo ambae
alishindwa kumpata yule mama, kumbe yule mama anaongea kwa karibu sana na
mchungaji Max hivyo akampeleka Ndesa.
Mchungaji Max: Ilifika
mahali chama kiliacha majukumu yote kumpata yule mama kuongea na Ndesamburo,
yule mama alisema CHADEMA wanacheza mpaka waongee nami, alisema CHADEMA ni
waongo na wanafiki, kwanini watufanya mpaka tumekosa urais. Mpaka juzi nilikuwa
nawasiliane nae lakini maongezi yake kwa ujumla anasema kwanini wameachwa
kugombea Urais, kwa jinsi alivyokuwa anaongea nikajua hata Dokta hawezi
kuchomoka.
Slaa alisema Josephine amemfungia Serena, ukweli mimi naufahamu, ishu ipo kwa
mkewe, Dr tumeshampoteza.
Gwajima: Siku moja nilikuwa Korea, Slaa alisema mkewe amedondoka amezimia,
nikaomba kwenye simu mkewe akaanza kupiga kelele, nilimwambia Dr. Slaa sijawahi
kuona mambo haya. Nilikuwa namsindikiza mke wangu kwenda London, cha kushangaza
nikamkuta mke wa Dr Slaa airpot amekuja kusindikiza, umeambiwa na nani! Akasema
nimejisikia tu! Baada ya check in, kurudi mke wa Dr. Slaa alidondoka chini,
mashetani yalikuwa yanamrudia.
Siku nyingine Slaa alinipigia simu mkewe amedondoka, haya ni mashetani, Slaa
anaongozwa na mwanamke wa aina hii. Ikulu pangekalika? Slaa si yeye, kuna
tatizo limetokea.
Slaa Serena alisema kwenye mkutano wa CHADEMA watu waliletwa na malori na
mabasi, mlioenda mjiulize ni kweli? Mtu anaesema uongo wa mchana, anasema
Gwajima anasema maaskofu wa katoliki wamepewa hela. Kanisa katoliki ndio kanisa
credible sana duniani.
Kwanini Slaa amesema! Kwanza kuwaondolea credibility, maaskofu hawa
wamemsomesha, leo maaskofu 30 anawasingizia. Kwa mtu unaemuamini Slaa unaweza
kusema anasema kweli lakini nimekuonyesha mazingira kwanini!
Anatukana maaskofu wa protestant na katoliki, nani aliemtuma! Slaa aliulizwa
unalindwa na usalama wa taifa? Alisema kweli, watu wa usalama wanambeba kwenda
Serena, Azam na Star Tv kutukana maaskofu. Maaskofu hawaruhusiwi kujihusisha na
siasa lakini ni wapiga kura, Je, atakupa kura! Je waumini wao watakupa kura!
Strategy hii imeshindikana wafikirie nyingine. Bahati mbaya hii ilikuwa silaha
yao ya mwisho.
Mababa askofu wa kanisa katoliki hawakupewa rushwa wala mimi sijapewa rushwa,
anasema nilikuwa nazunguka kwenye ndege na Lowassa. Mimi nina ndege yangu na
siombi kibali kuzungumza mtu.
Usalama wa taifa sio wa CCM, mnatafasiriwa nyie ndio mnatukana maaskofu,
usalama wa taifa mnamuharibia Magufuli, mwacheni aendelee kampeni zake kwa
amani.
Siku nitakayorudi kumjibu Slaa akinisemesha, nitasema Slaa alivyokutana na watu
wa usalama wa taifa Afrika kusini. Usalama mtapomuongoza tena huyo mtu wenu
wenu atukane maaskofu, nitawalipua na bomu na macho yenu hamtafungua tena
Uadalifu wa Slaa
Gwajima: Alisema baba
askofu lazima mtubu, najiuliza yeye ni msafi kuliko sisi? Slaa aliacha wito
ambalo ni tatizo tayari, zaidi ya kuacha wito ukaoa! Nikija tena nitaleta
watoto aliowazaa na uhusiano wa yeye kutoka. Ukaa na mke na watoto ukatelekeza,
haitoshi ukaenda kuoa mke wa mtu mwingine. Kamili akaweka zuio mahakamani.
Slaa alisema Ridhwani nauza madawa ya kulevya, leo Slaa ndio anao aliowasema,
anaemuongoza Slaa akome na akome kabisa. Watu wa usalama kazi yenu ni kulinda
nchi iwe na amani na sio kuichafua.
Kinachosumbua ni wakati na majira, 20 kabla ya kristo kulikuwa ana mtu
aliehubiri ubudha, akaijaza Ubudha kwa sababu yalikuwa majira yake. Baada ya
hapo, karne ya kwanza alitokea Yesu kristo na kukutana na upinzani wa ajabu,
ukifika wakati waksema wamemkamata.
Kweli ukiizika ina tabia ya kufufuka na ukiizika haiwezi kufa tena, akaja
kutokea Mtume Muhammad japo alipata upinzani mkubwa leo Uislam umeenea sana.
Nami niseme mfate majira, msishindane nayo. Tanzania ni kubwa kuliko
watanzania.
No comments:
Post a Comment